Sheikh Shariff Matongo
akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)kuhusu ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka
2015.
NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII, DAR
Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015
na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali duniani ambavyo vitatokea nchini na
viongozi wasipuuze ndoto hiyo.
Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo katika uchaguzi ujao wa Tanzania kupatikana Rais ambaye ni kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.
Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo katika uchaguzi ujao wa Tanzania kupatikana Rais ambaye ni kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.
Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh alisema ndoto nyingine kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi
mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata
mafanikio makubwa kwa mwaka utaoanza
kesho.
Vijana wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee
wataangushwa sana ihivyo wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa itapita lakini kutakuwa na vurugu ambazo
zitaibuliwa na vijana.
‘’Ndoto yangu
niliopoteshwa sikukaanyo peke yangu niliweza kupata ushauri kutoka kwa
watu mbalimbali akiwemo Mufti wa wa Abuu Dhabi,Mufti wa Nigeria na wengine wote wanakaniambia suala hilo
nisikaaye nalo nishirikishe na watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff
Matongo.
Sheikh Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa
mbaya kutokana na bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na
kuchafuka huko.
Alisema ndoto hizo ni lazima kuweza kuzingatia kutokana na
kupata ushauri wa watu wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa
mbalimbali ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269