Serikali
imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha
kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika kuchangia
kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14,
mwezi huu.
Akitangaza
hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika
uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia
umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao
waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu,
Serengeti, Sengerema na Bunda, waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa
Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na wa Manispaa ya Sumbawanga.
Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo
kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine watatu wakipewa
onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269