Breaking News

Your Ad Spot

Jan 19, 2015

AJIRA ZA VIJANA WANAOAJIRIWA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZAONGEZEKA

Katibu Mkuu Msaidizi, Idara ya Ajira Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Malimi Muya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa kuhusu kuongezeka kwa vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa umma. Kushoto ni Ofisa Habari, Kassim Nyaki.
Ofisa Habari wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kassim Nyaki (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. 
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema ajira za vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa Umma imeongeza kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2010-2014 huku wanawake wakionesha kuongoza.

katika hatua nyingine serikali  inatarajia kuajiri vijana 7,210 nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015-2016.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi  Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma     Umma, Malimi Muya, alisema nafasi za ajira 7,210 zimetengwa kwa  ajili ya vijana wa kitanzania.

"Tunatarajia kuongeza ubunifu na ufanisi mkubwa katika sekretarieti ya ajira kwa sababu tunaamini vijana wana uzoefu wa kutumia  vifaa vya teknohama," alisema

" Takwimu zinaonesha kunaongezeko la ajira kwa vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa umma kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2010-2014 huku wanawake wakiongoza.

Tangu Sekretarieti ya ajira kuanza mchakato wa ajira katika Utumishi wa umma tumepokea jumla ya maombi ya kazi 191,844 kati ya hayo waliyoita kwenye usahili walikuwa waombaji 71,124.

"Hadi kufikia Desemba 2014 jumla ya waombaji kazi 12,858 walipangiwa vituo vya kazi na kati ya hao wanaume walikuwa 7,598 sawa na asilimia 59.1,wanawake walikuwa 5,260 sawa na asilimia 40.9," alisema Muya.

Katika waajiriwa 12,858 waliopamgiwa vituo vya kazi vijana wenye umri wa miaka 26-30 walikuwa 6,346 sawa na asilimia 49.5 kwa msingi huo ndani ya miaka mitatu utumishi wa umma umeajili vijana mwenye ongezeko la asilimia 57.5,"alisema.

Muya alifafanua kuwa idadi ya wanawake walioajiliwa katika utumishi wa umma imekuwa ikiongezeka kutoka mwaka hadi mwaka.

"Mwaka 2010 wanawake walioajiliwa katika sekretarieti ya ajira walikuwa  aslimia 27.7 wakati mwaka 2013-2014  wanawake walifika 49.4 hili ni sawa na ongezeko la asilimia 41.1 wakati wanaume wakiwa na ongezeko la asilimia 27.9,"alisema.

Katibu msaidizi huyo,alitoa rai kwa wanafunzi  kuyapenda masomo ya sayansi ili kusaidia tumme kupata watalamu wa sayansi kwani tume inauhaba mkubwa wa watalamu wasayansi.

"Tumme inauhaba wa watalamu wa sayansi kama vile wahandisi wa petroli,watalaam wa mifugo,wahandisi wa kilimo na wengine wengi,"alisema.

Aidha katibu huyo alisema aliotuma maombi ya kazi na kufanyiwa usahili Desemba 2014 tangazo la kupangiwa vituo vya kazi litatolewa kabla ya mwisho wa mwezi Januari kuisha.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages