Na Fatuma Bashir
IKIWA ni mwaka mmoja sasa tango utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN imeelezwa kuwa hali ya utekelezaji huo bado si ya kuridhisha.
Imeelezwa kwamba baada ya ya mwaka 2013 Serikali ya Tanzania kuzindua mpango maalum wa ufuatiliaji utekelezaji wa mipango na na utoaji wa huduma kwa umma unaojulikana kama BRN, kwa lengo la kusukuma maendeleo na kuharakisha utekelezaji mipango na kuleta matokeo yaliyokusudiwa upesi kama hatua ya mwanzo ya BRN, ilichagua sekta sita za mfano ambazo ni Kilimno. Maji, Elimu, Nishati na madini, Fedha na Usafirishaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Elimu, Bwana Godfrey Boniventura alisema, licha ya serikali kuanza kufanya na kutoa tathmini ya mpango huo kupitia jopo la Kimataifa la Tathmini (IRP), Taasisi hiyo kama mdau wa Elimu imefanya tathmini yake ili kupima ufanisi wa matokeo ya mpango huo katika sekta hiyo ya elimu kwa mwaka mmoja na kubaini kwamba matokeo bado si ya kuridhisha.
Alisema, katika sekta ya elimu yaliyopangwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja kati ya 2013/14, ni pamoja na kuongeza ufaulu hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2014, kutoa ruzuku iliyopamgwa kwa kila mwanafunzi, kutoa mafunzo ya uongozo kwa walimu 19035 kufikia Septemba 2013, mafunzo kwa walimu 12300 juu ya ufundishaji wa KKK, kujenga nyumba 500 za walimu kwa shule za sekondari.
Mengine ni kukarabati miundombinu kwa shule 1200 za sekondari na kuhakikisha kuwa uwiano wa mwanafunzi kwa kitabu unashuka kutoka kitabu kimoja kwa wanafunzi watano hadi vutabu sita kwa mwanafunzi mmoja.
Biniventura alisema japokuwa taarifa ya jumla ya jopo la IRP, inasema mwelekeo wa utekelezaji wa BRN ni mzuri, katika ufuatiliaji uliofanywa na Haki Elimu katika sekya ya elimu kwa karibu sana imebaini kuwa hali ya utekelezaji wake bado si ya kuridhisha.
"Mathalani BRN ilipamnga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za sekondari na msingi hadi kufikia asilimia 60 mwaka 2013 na silimia 70 mwaka 2014, pamoja na matokeo kuonyesha matokeo kuonyesha ongezeko la ufaulu kutoka asilimia 50.6 (2012) hadi kufikia asilimia 50 (2013) kwa shule za sekondari na kutoka asilima 30.7 mwaka 2012 hadi asilimia 50.6 mwaka 2013 kwa shule za msingi, bado lengo la asilimia 60 halikufikiwa", alisema Biniventura na kuongeza kuwa,
"Hali hiyo inaonyesha kuwa lengo la ufaulu kwa shule za sekondari kufikia asilimia 60 kwa mwaka 2013 limefanikiwa kwa asilimia karibu 79 na kwa asilimia 42 tu kwa shule za msingi".
Alisema hata hivyo ufaulu wa sekondari siyo wa kujivunia kwa sababu matokeo ya mtihani wa mwaka 2013 yametumia viwango vipya vya madaraja na hivyo haiwezekani kusema yametokana na utekelezaji wa BRN.
Boniventura alisema kwa upande wa ruzuku BRN, imeshindwa kufikia lengo la kupeleka ruzuku iliyokamilika katika mwaka wa fedha 2013/14 wakati shule za msingi zilipaswa kupokea wastani wa sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi lakini ni wastani wa sh. 3580 tu kwa kila mwanafunzi uliofika shuleni na wastani wa sh. 16, 384 tu ukifika shule za sekondari badala ya sh. 25,000 uliopangwa.
Alisema mwenendo huo wa utoaji ruzuku siyo dalili tu za kuyofikiwa malengo ya BRn bali pia ni ishara hasi ya kufikia lengo la kuboresha elimu hapa nchini kwa sababu ruzuku ya wanafunzi ndicho chanzo kikuu cha mapato kwa shule za umma ambapo hutumika kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kukidhoi gharama ndogondogo za uendeshaji wa shule hivyo shule zimapokosa ruzuku zinashindwa kunoresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia na hivyo kuathiri ubora wa elimu itolewayo shuleni.
Boniventura alisema BRN pia ilikuwa imeazimia kuwa hadi kufikia Septemba 2014 serikali itakuwa imefanya ukarabati na ujenzi wa miundombinu kwa shule 792 lakini hadi kufikia Machi 2014 ni shule 56 tu ndizo zilikuwa zimefanyiwa ukarabati.
Alisema licha ya BRN kujikita katika ujenzi na ukarabati miundombinu lakini changamoto ya ubovu wa miundombinu bado ni kubwa kwa shule nyingi, takwimu za BEST, 2014 zinaonyesha kuwa wa shule za sekondari kuna upungufu mkubwa wa maabara 1355 sawa na asilimia 94.8, za kilimo, maabara 4416 za baiolojia sawa na asilimia 76.4, maabara za kemia 4461 sawa na asilimia 72.6 na maabara za Fiizikia 1024 sawa na asilimia 75.
Pia kuna upungufu wa nyumba 51187 za walimu sawa na asilimia 72, madarasa 13591 sawa na asilimia 22.6 na matundu ya vyoo 44926 sawa na asilimia 40, hali ikiwa mbaya zaisi kwa shule za msingi ambapo kuna upingufu wa vyoo 27,736 sawa na asilimia 60.3 ambapo uwiamo wa wanafunzi wa tundu la choo ni 1:53 badala ya 1:23 kwa wavulana na 1:51 kwa wasichana badala ya 1:20.
Alisema, pia kuna upunguzu wa madarasa 82,788 sawa na asilimia 41 ambapo uwiano wa wanafunzi kwa darasa ni 1:72 na tatizo ni kubwa zaidi kwa mikoa ya Rukwa uwiano 1:84, Geita 1:126 na Mwanza 1:110, upungufu wa nyumba za walimu 16,007 sawa na asilimia 79 na madawati milioni 1.2 sawa na asilimia 37.7.
Boniventura alisema, serikali pia ilikusufdia kutoa mafunzo kwa walimu 19, 350 kwa shule za msingi na sekondari hadi ifikapo Septemba 2013 lakini taarifa za utekelezaji zinaonyesha kuwa hadi kufikia Aprili 2014 serikali iliweza kuwapatia mafumzo ya uomgozi walimu 3469 tu ambao ni wa shule za sekondari na hivyo kuwa imetekeleza lengo hilo kwa asilimia 18 tu.
Alisema changamoto kubwa inaonyesha kuwa walimu wa shule za msingi ambao hadi kufikia Septemba 2014 hakuna hata mwalimu aliyepatiwa mafunzo ya uongozi kati ya walimu 15,524 waliotarajiwa kupatiwa mafunzo hayo.
Your Ad Spot
Jan 22, 2015
Home
Unlabelled
HAKIELIMU: UTEKELEZAJI WA BRN KATIKA ELIMU BADO HAURIDHISHI
HAKIELIMU: UTEKELEZAJI WA BRN KATIKA ELIMU BADO HAURIDHISHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269