Na MatukiodaimaBlog
MKOA wa mbeya umepania kuboresha miundo ya kituo cha mambo ya kale cha Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa iwapo Idara ya Mambo ya kale iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali ombi la mkoa huo kukabidhi kivutio Halmashauri ya Mbozi.
Hatua
hiyo imekuja kufuatilia ziara ya wanahabari mkoani Iringa
wanaotembelea vivutio vya utalii mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa
kama njia ya kuhamasisha utalii mkoa ya nyanda za juu kusini na
pia kubaini sababu za utalii kutokua kwa kasi katika mikoa hiyo .
Mhifadhi
msaidizi wa kituo cha makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo
wilayani Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema kuwa mbali ya watalii wengi
kupenda kutembelea eneo hilo la Kimondo ila miundo mbinu ya eneo
hilo si rafiki kwa watalii kuendelea kutembelea kutokana na
serikali kushindwa kuboresha majengo na eneo hilo kwa ujumla.
Alisema
kuwa kimondo hicho ambacho mwaka kilipoanguka eneo hilo
haufahamiki ila utafiti wake ulianza kati ya mwaka 1930 -1931 na
kubainika kuwa si jiwe la kawaida bali ni sayari iliyoanguka kutoka
angani toka wakati huo kimendelea kupata umaarufu wa watalii
kufika kutembelea eneo hilo japo katika eneo hilo mazingira yake ni
mabovu zaidi.
Mhifadhi
huyo akielezea historia ya kimondo hicho alisema kabla ya
watafiti kubaini kuwa ni kimondo miaka ya nyuma kulikuwa na
wenyeji ambao walikuwa wakiishi eneo hilo na mkazi mmoja
aliyefahamika kwa jina la Harele ambae alikuwa akifanya kazi ya
uhunzi kuweza kubaini jiwe hilo la ajabu wakati akitafuta udongo chuma
kabla ya kumega kipande kidogo na kutengenezea shoka .
Alisema
kutokana na wakati huo chuma kuwa na dhamani kubwa alipeleka
taarifa kwa chifu wa eneo hilo na kulifanya eneo hilo kuwa la
tambiko kabla utawala wa Waingereza kuchukua eneo hilo na
kulihifadhi kabla ya serikali ya Tanzania kupitia idara ya mambo ya
kale kuhifadhi eneo hilo.
Kuhusu
changamoto kubwa zilizopo eneo hilo alisema ni pamoja na kukosekana
kwa nyumba bora za watumishi ,jengo la ofisi ya makumbusho kutokana
na kibanda kilichopo kutokuwa na sifa ya utalii ,pia miundo mbinu ya
barabara kufika kituoni hapo.
Afisa
utalii ofisi ya utalii kanda ya kusini Bi Risala Kabongo akielezea
kivutio hicho alisema kuwa ni moja kati ya vivutio visivyo vya
kawaida hapa nchini na kuwa iwapo serikali itaboresha zaidi eneo
hilo upo uwezekano wa uchumi wa mkoa wa Mbeya kukua zaidi kupitia
kivutio hicho .
"
Kivutio hiki kinavutia zaidi ila ushauri wangu kwa serikali ni
kuboresha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na kutenga eneo la banda la
wageni na eneo la kujenga mahema kwa wageni.....Kimondo hiki kimetoka
katika sayari ya Mars na hivyo ni kivutio cha ajabu zaidi"
Katibu
tawala msaidizi (miundombinu) mkoa wa Mbeya Kastory Msigala
alisema kuwa mkoa huo kupitia kikao chake cha kamati ya ushauri
ya mkoa kimeiandikia barua idara ya mambo ya kale ili kuipa eneo
hilo la Kimondo Halmashauri ya Mbozi ili kusimamia kwa lengo la
kuiboresha zaidi.
Kwani
alisema shida kubwa ya Halmashauri hiyo na mkoa kushindwa
kuboresha majengo na miundo mbinu inayozunguka makumbusho hayo ni
kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kutokana na usimamizi
wa eneo hilo kuwa chini ya idara ya mambo ya kale ila pale idara
hiyo itakapokabidhi katika serikali ya wilaya upo uwezekano wa
wilaya kusimamia vizuri zaidi.
Alisema
katika mkoa huo kuna jumla ya vivutio 13 vilivyotambuliwa
kikiwemo kivutio hicho cha Kimondo na kuwa mbali ya vivutio
hivyo bado mkoa umejipanga zaidi kutangaza utalii kufuatia
ushirikiano mkubwa uliopo kati ya mkoa huo na ofisi ya SPANEST , bodi
ya utlii ,wizara ya utalii na wadau mbali mbali kukuza utalii
mkoani humo .
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269