Mwakilishi wa Kudumu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, jana Ijumaa alijumuika na wawakilishi wa Kudumu wa Mataifa mengine katika Umoja wa Mataifa, waliojitokeza katika kile kinachoweza kuelezwa kama mshikamano kusaini kitabu cha Maombelezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Ufarasa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio linaloelezwa kuwa la kigaidi lililotokea siku ya Jumatano
ambapo watu kumi na mbali wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo walipoteza maisha katika shambulio hilo.
Pichani, Balozi Tuvako Manongi akibadilishana mawazo na Mabalozi wenzie muda mfupi kabla ya kusaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio la jumatano ambapo watu kumi na mbili wakiwamowaandishi wa gazeti la Charlie Hebdo walipoteza maisha
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akiandika salamu za rambirambi kufuatia tukio linaloelezwa kuwa la kigaidi ambapo watu kumi na mbili wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo waliuawa
Your Ad Spot
Jan 10, 2015
Home
Unlabelled
TANZANIA YAOMBELEZA NA WAFARANSA
TANZANIA YAOMBELEZA NA WAFARANSA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269