Meneja wa kiwanda cha pareto mafinga (PCT) Martine Oweka
mkulima akiwa shambani akiendelea kufanya kazi shambani.hili ni shamba lilopo mbeya
wakulima wakiwa shambani wakiendelea kufanya kazi shambani huko mbeya.
hii ndio pareto yenyewe ikiwa tayari kwa kuvunwa
KIWANDA
cha Pareto (PCT), cha Mafinga wilayani Mufindi kimetumia zaidi ya shilingi
milioni 400, kwa ajili ya kuwasaidia wakulima mbegu na miche ya zao hilo, ili
kukuza na kuinua zao hilo.
Kila
msimu wa Kilimo, kiwanda hicho kimekuwa kikisambaza mbegu na miche ya Pareto kwa
wakulima wa zao hilo katika mikoa yote ambayo zao hilo limekuwa likistawi
ikiwemo Iringa, Mbeya, Njombe na Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Meneja wa kiwanda hicho Martine Oweka alisema kuwa
lengo lao ni kuhakikisha zao la Pareto ambalo ni mkombozi kwa mkulima.
Oweka
amewataka wakulima wa mikoa hiyo kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kuinua kipato chao na kuondokana na umaskini
kutokana na kuwepo kwa uhakika wa soko la zao hilo, tofauti na miaka ya
nyuma kufuatia uwepo wa kiwanda.
Oweka
alisema ili wakulima waondokane na umaskini, lazima wajikite katika mazao ya
biashara likiwemo pareto, kutokana na zao hilo kwa sasa kuwa na bei nzuri
katika soko la dunia.
Alisema
kuwa endapo wakulima wa mkoa wa Iringa na mingine inayostawisha zao hilo
wataamua kulima pareto kama zao mama la biashara wanaweza kuondokana na
umaskini, kutokana na ukweli kwamba, zoko la pareto limekuwa na uhakika tofauti
na miaka ya nyuma wakati soko la zao hilo lilipoyumba.
Aliongeza
kuwa kwa sasa kiwanda chao kinalima zaidi ya ekari 300 za pareto, na
kwamba kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa wakulima wanalima zao hilo na
kufuatilia hatua zote za kupanda, kuvuna, kukausha na kusafirisha hadi
kiwandani.
Akizungumzia masoko ya kimataifa Oweka alisema kuwa kwa sasa zipo nchi nyingi ambazo zinauhitaji mkubwa wa zao la pareto na ndiyo maana bei yake ipo juu.
Akizungumzia masoko ya kimataifa Oweka alisema kuwa kwa sasa zipo nchi nyingi ambazo zinauhitaji mkubwa wa zao la pareto na ndiyo maana bei yake ipo juu.
Alizitaja nchi hizo kuwa ni Japani, India, Australia na nchi zilizopo bara la Ulaya kuwa wananunua pareto kwa wingi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269