Mhubiri mmoja huko Brazil, Alex Novais de Brito aliyekuwa
akifanya mahubiri kwenye mazishi ya muumini wake amejikuta akishindwa
kumaliza ibada hiyo baada ya udongo wa kaburi kudidimia na kufanya
Mchungaji huyo na waumini wengine watatu kudumbukia kwenye kaburi.
Hilo lilitokea kwenye makaburi ya Campo da Esperanca wakati kukifanyika ibada ya mazishi.
Watu
wawili walipelekwa Hospitali ya jirani ili kutibiwa majeraha madogo
waliyoyapata baada ya kuanguka, watu walichanganyikiwa baada ya kutokea
tukio hilo, Mhubiri huyo alijikuta kwenye wakati mgumu na kushindwa
kumalizia ibada.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269