Na Makongoro Oging’, Issa Mnally/Uwazi
MTU
mmoja anayeaminika kuwa ni Mtanzania, Robert John Mpwata (34) anadaiwa
kuuawa kwa kuwekewa sumu na mwili wake kukutwa chumbani kwake katika Mji
wa Shorten nchini Ujerumani siku chache zilizopita.
Habari
kutoka kwa baadhi ya marafiki zake waliopo huko, zinasema Robert
aliyekuwa mwanamichezo aliyecheza sarakasi, karate na judo, aliwasiliana
nao kwa njia ya simu mara kwa mara na walipata taarifa za kifo chake
siku saba ya kufariki dunia.
Inadaiwa
kabla ya kifo cha mwanamichezo huyo, alikuwa akiwasiliana vizuri na
wenzake, lakini umauti wa ghafla uliomkuta na mazingira yake, unawapa
hofu kuwa huenda alifariki baada ya kuwekewa sumu.
Inadaiwa
kuwa Februari 8, mwaka huu ilikuwa ni siku waliyotakiwa kufanya
onyesho, kitu ambacho kiiwafanya wawe na mawasiliano ya mara kwa mara.
Mwandishi
wa habari hii aliwasiliana na ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani,
ambako mfanyakazi mmoja aliyekataa kutajwa jina lake kwa vile siyo
msemaji, alikiri kusikia taarifa hizo, lakini akasema inakuwa vigumu
kwao kutoa msaada kwa vile taarifa isiyo rasmi inasema marehemu alikutwa
na vielelezo vinavyomtambulisha kuwa ni mtu wa Somalia.
Robert John Mpwata akiwa na mke wake.
Naye
Mwenyekiti wa umoja wa Watanzania nchini humo, Mfundo Peter Mfundo
alikiri kutokea kwa kifo hicho, kwani awali marehemu aliwaaga Watanzania
wenzake kuwa ataondoka kwenda nyumbani kwa mke wake.
“Mimi
nilipata taarifa kutoka kwa rafiki yake wa karibu baada ya wiki mbili
tangu akutwe amefariki, hakuna anayejua kilichomuua maana serikali bado
haijatoa majibu. “Mpaka sasa bado tunasubiri kutatokea nini na hata kama
ikitokea tupewe maiti kuisafirisha ni kazi kwani ni zaidi ya shilingi
milioni 12, nimewasiliana na baba yake anasema hana nauli ya kumleta
huko.
“Robert
alikuja hapa katika shughuli za sanaa na alimuoa Mjerumani aliyezaa
naye mtoto Daniel ambaye ana umri wa miezi minne,” alisema kiongozi
huyo.Kwa mujibu wa Peter, mke wa marehemu aliwaambia kwamba angependa
amzike mumewe nchini humo ili iwe rahisi kwa mtoto wake kuhani kaburi
lake.
John
Mpwata (65), baba mzazi wa marehemu akiwa nyumbani kwake Manzese
Kilimahewa jijini Dar, alisema taarifa za kifo hicho
zimemuumiza.“Mwanangu aliondoka mwaka 2007 kutafuta maisha huko
Ujerumani na kwa mara ya mwisho niliongea naye Desemba 22, mwaka jana,
aliniambia atakuja nyumbani na mkewe Mzungu hivi karibuni baada ya
mwanaye Daniel kuanza kutembea.
“Lakini
cha kushangaza hivi karibuni nimepata taarifa ya kifo chake, sina jinsi
maana nimeambiwa uwezekano wa mwili kuletwa ni mdogo na ningependa
kwenda kumzika lakini sina milioni 2.5 za nauli, ninawaomba Watanzania
wanisaidie nikamzike mwanangu,” alisema na kutaja namba zake za simu
kuwa ni 0689 476408 au 0713 432088.
Credit: Gpl
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269