Wafanyakazi wa Kampuni ya Majinjah
Logistics Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka kushoto mstari wa
mbele (wa pili) Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin
Mwandete,Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu
(NIT),Dk,Ethel Kasembe,Mhandisi, Charles Kisunga na Dereva wa kike wa
Majinjah,Grace Andrew.
Wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa
Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wao na viongozi wa NIT.
Mhandisi, Charles Kisunga wa NIT
akizungumza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah
Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho
na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe (wa pili kulia) na
Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona,
Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na
Masomo ya Elimu ya Juu,Dk,Ethel Kasembe (kulia) akizungumza kabla ya
kukabidhi vyeti wahitimu.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete na Mhandisi, Charles Kisunga wa
NIT.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) akitoa nasaha kwa wahitimu.
Mwalimu wa Madereva, Daniel Kasisi,akifuatilia utoaji wa Vyeti kwa Wahitimu 21 wa Maginjah Logistics Ltd.
Na Mwandishi Wetu
Madereva 21 wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wamepatiwa mafunzo ya siku tatu katika Chuo cha Taifa cha Usafirishji (NIT).
Mafunzo hayo yalihusu Alama na Michoro
ya barabarani,Sheria,Udereva wa Kujihami,Vyanzo vya Ajali jinsi ya
kuzizuia,Huduma kwa Wateja na mawasiliano ya Barabarani.
Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na
Masomo ya Elimu ya Juu, Dk,Ethel Kasembe,aliwaambia madereva kuwa elimu
waliyoipata itawasaidia kuepusha ajali za barabarani wakati wakiendesha
mabasi yanayobeba abiria na kuwataka waendelee kupata elimu ya kutosha.
Alisema kuwa imani yake takwimu za ajali
zitapungua na hata kwisha kabisa kama watazingatia waliyofundishwa na
kuwasisitiza kwenda Chuoni hapo mara kwa mara kuendelea kupata elimu.
Pia alisisitiza kuwa watabadilika baada
ya kumaliza mafunzo ya hapo na kuwa vyanzo vya ajali watavizuia kwa
kutumia udereva wa kujihami wakiwa barabarani wakati wote
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269