Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Seti za Jezi na
Mipira Mmoja wa Viongozi wa timu 60 zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope
hapo Kijiji cha Kipandoni Upenja Wilaya ya Kaskazini “B”. Katikati yao ni Mke wake Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
Baadhi
ya vijana wa timu za mitaani zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope
zilizopata vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo,
Balozi Seif Ali Iddi, wakiwa katika hafla hiyo.
Kocha
na Kepteni wa Timu ya Soka ya Kipandoni Star Jeilan Omar Jeilan
akipokea mchango wa shilingi 500,000/- kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la
Kitope Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kununulia Posi na Nyafu kwa
ajili ya Kwinja chao cha michezo. (Picha zote na – OMPR – ZNZ)
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/3/2015.
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi leo amekabidhi vifaa vya
michezo kwa Timu 60 za Mpira wa soka zilizomo ndani ya Jimbo hilo ili
kusaidia nguvu na chachu ya kuimarisha Michezo katika Jimbo la Kitope.
Vifaa
hivyo ambavyo ni seti za Jezi na Mipira vyenye Thamani ya shilingi
Milioni Nane, Laki Nne na Hamsini Elfu { 8,450,000/- } vimekabidhiwa
kwa timu hizo hapo Kipandoni Wadi ya Upenja Wilaya ya Kaskazini “B”.
Balozi
Seif akiambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya
Viongozi wa Wadi ya Upenja na Jimbo la Kitope akikabidhi Seti za Jezi na
Mipira kwa Timu za Jimbo hilo zinazoshiriki Ligi ya Kanda ya
Unguja,Daraja la Pili na daraja la Tatu.
Na
pia akakabidhi mipira kwa 36 ya Mitaani pamoja na timu mbili za watoto
wadogo wa Kijiji cha Kipandoni na kuahidi kuonyesha nia ya kusaidia
kuwatengenezea Kiwanja watakachokichaguwa ili kiwe na hadhi ya michezo
ya Kitaifa ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.
Akizungumza
na Wanamichezo hao Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi
aliwataka Vijana hao kujiepusha na makundi ya baadhi ya watu
wanaojaribu kuwashawishi wajiingize katika mambo yaliyo nje ya Sekta ya
Michezo.
Balozi
Seif alisema ni vyema kwa vijana hao wakaendelea kuwaamini Viongozi
waliokubali kuwatumikia katika mambo na harakati zao za kila siku hasa
zile za michezo ambazo kwa sasa husaidia kutoa ajira.
Aliwataka
wanamichezo hao kupitia Viongozi wao waangalie utaratibu wa kutafuta
kiwanja kitakachowekewa miundo mbinu ambayo baadaye kitakidhi mahitaji
ya kuchezewa Ligi yenye hadhi ya Kitaifa.
Mapema
Mke wa Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi alisema
katika kuunga mkono juhudi za wanamichezo hao alisema ni vyema kwa
wanasoka hao wanzishe utaratibu wa kuanza kuchangia hata kwa kiwango
kidogo ili kuwapa nguvu Viongozi na wafadhili wanaoonyesha nia ya
kuwasaidia.
Mama
Asha alisema Viongozi wa Jimbo hilo watashawishika na kuongeza nguvu
zao kwa Timu ambazo tayari zimeshajikubalisha kujisaidia zenyewe
zikisubiri nguvu za ziada.
Mapema
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar Wilaya ya Kaskazini “
B” Tongoa Moh’d Hassan alisema Wilaya hiyo bado inakabiliwa na
changamoto kubwa ya ukosefu wa Kiwanja cha soka chenye hadhi
inayokubalika kwa michezo mikubwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269