MJI wa Songea jana ulizizima kwa
mapokezi makubwa ya viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakiwa na kiongozi wa chama hicho, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, aliyeachana na Chadema hicho hivi karibuni baada ya kuwepo mzozo mkubwa baina yake na viongozi.
Viongozi wengine wa juu wa ACT walioambana na Zitto ni pamoja na Mwenyekiti wa ACT Taifa, Anna
Mghwira na Katibu Mkuu wake Samson Mwigamba.
Baada ya kuwasili mjini
hapa walilakiwa na mamia ya wananchi wa mji wa Songea
wakiongozwa na vijana zaidi ya 300 wa bodaboda.
Akihutubia mamia ya wananchi
hao mjini Songea katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa
Stendi ya Malori Majengo, Zitto, alisema lengo la kuanza ziara mkoani
Ruvuma ni kuenzi na kutekelza kwa vitendo azimo la Songea.
Alisema na hilo pia mkoa huo una
historia ya ukombozi wa vita ya majimaji iliyoanzia wilayani Kilwa na
baadaye kuenea hadi Songea.
Mbunge huyo wa zamani ya Kigoma
Kaskazini, alisema kutokana na hali hiyo ACT-Wazalendo wameanza ziara
hiyo ili kupata baraka za mababu wa ukombozi na si kushindana au
kuviponda vyama vingine vya siasa.
Alisema kitendo cha baadhi ya
watu kufikiri kuwa ziara yake ina lengo la mashambulizi si sahihi bali
sasa ni changamoto kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanapanda
viongozi wa upinzani kama njia ya kustawisha demokrasia nchini.
“Ruvuma ni Mkoa ambao hauna
mbunge wa upinzani hata mmoja na tumeona tutume salamu kwa umma huku
lengo letu likiwa likiwa kuing’oa CCM madarakani na kwamba hatuna nia ya
kugambana na vyama vingine.
“Wakazi wa Songea ni wajibu wenu
kupima je pamoja na historia ya ukombozi ambayo ACT-Wazalenzo tunaamini
ndio misingi ya ukombozi wan chi yetu je kukosa mbunge hata mmoja wa
upinzani ni sahihi, hili ni lazima tulikate na tufanye uamuzi huo sasa
hasa kuelekea Oktoba mwaka huu,” alisema Zitto.
Akizungumzia Mkoa wa Ruvuma kama
mmoja wa mikoa mitano inayotegemewa kwa uzalishaji mkubwa wa chakula,
alisema pamoja na wakulima kuhangaika usiku na mchana lakini bado hakuna
juhusu za Serikali za kuwakomboa katika lindi la umaskini ili wafurahie
kilimo chao.
Alisema kwa muda sasa bei za
mazao zimekuwa zikishuka lakini bado Serikali imeshindwa kuwalipa
wakulima Sh bilioni 13 za mahindi bila kuwa na utaratibu madhubuti wa
kulipa madeni hayo.
“Kwan chi zilizoendelea zimekuwa
zikithamini juhudi zinazofanywa na wakulima ikiwemo kuundiwa mfuko wa
mazao, ambao unafanya kazi ya kuhakikisha dhamani ya mazao inalindwa.
“Ikitoa bei ya mazao inashuka
linakua jukumu la mfuko kulipa fidia ya hasara kwa wakulima, ambapo
hili huenda sambamba na kuwepo kwa mfuko huo ambao
“Nasi ACT- Wazalendo tungependa
kuonyesha sera yetu ya hifadhi ya jamii ambapo kila mkulima awe na bima
ya afya. Mpango wetu ni kwamba kama mchango wa hifadhi ya jamii ni Sh
30,000 basi Serikali itamchangia mkulima Sh 10,000,” alisema Zitto.
Alisema kutokana na changamoto
za wakulima wanataka kuonyesha wana majawabu ambapo mkulima atatibiwa
bure akiwa na hifadhi ya jamii na uhakika wa bei kupitia mfumuko wa bei
katika hifadhi ya jamii.
“Utafiti wa Shirikala la Kazi
Duniani (ILO), wa mwaka 2013 unaonyesha kuwa nchi ambazo zimesambaza
hiafdhi ya jamii kwa wananchi wake wote zimeondoka kwenye umaskini kwa
kasi na ukiaji wa uchumi unaongezeka mara dufu,” alisema Kiongozi huyo
wa ACT-Wazalendo.
Mgomo wa madereva
Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma
Kaskazini, alisema kuwa kilichotokea jana ni mapambano kati ya wenye
nguvu na wanyonge kwani madereva hawana mikataba ya kazi zao lakini
wamiliki wamekuwa wakiwanyonya madereva huku Serikali iksihindwa
kuchukua hatua zozote.
“Hatua za kuimarisha usalama
lazima ziendane na usalama wa ajira za Watanzania katika sekta ya
usafirishaji hivyo Serikali ichukue hatua za haraka kwa kukutana na
viongozi wa madereva na kupata suluhisho la kudumu.
“Waziri Samuel Sitta asitishe
kwa muda uamuzi wa Serikali kuhusu mafunzo na Serikali ihakikishe
madereva wote wana mikataba ikiwemo michango kwenye hifadhi ya jamii,
Serikali itekeleze uamuzi wa mafunzo.
“Kuna haja ya kuhakikisha kuwa
udereva wa mabasi ya abiria ni taaluma hivyo kuwepo na mfumo wa
‘accredition’ kupitia umoja wa madereva katika usafirishaji wa umma,”
alisema.
Zitto alisema ACT-Wazalendo,
inasimama upande wa wanyonge hivyo ipo na madereva wote nchini wanaovuja
jasho kuzalisha kwa ajili ya matajiri wao na pia tunaitaka Serikali
imalize tataizo hili mara moja na wananchi waendelee na shughuli za
uzalishaji kama kawaida.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, alisema chama chake hakina ugomvi na chama
chochote cha siasa nchini na kipo tayari kushirikiana na chama
kinachoamini katika itikadi za kitaifa.
“Ninajua hapa kuna watu wamekuwa
wakisema kuwa ACT-Wazalendo haitaki kushirikiana na vyama vingine hili
si kweli kubwa tunachosema kama kuna chama kinaamini katika misingi ya
ujamaa kije tutashirikiana nao,” alisema Anna.
Kabla yakuwahutubia wananchi
mjini hapa viongozi hao wa ACT-Wazalendo, alisema wakazi wa vitongoji
vya mji huo Zitto alifungua matawi kadhaa ya chama hicho ambapo
alielezea mikakati ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba mwaka huu.
Matawi yaliyofunguliwa jana katika eneo la Mshangano, Bombambili, Msamala kwa Mauki na Lizaboni.
Mbali na kufanya shughuli hizo
pia walitembelea makumbusho ya mashujaa mjini hapa pamoja na kufanya
vikao na viongozi wa chama na ngazi ya mkoa kama njia ya kujiimarisha.
PICHA ZA ZIARA HIYO YA ACT: BOFYA HAPA
PICHA ZA ZIARA HIYO YA ACT: BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269