Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR 248
katika mikoa saba nchni Tanzania Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.
Mikoa
iliyopangwa kuanza kupokea mashine hizi ni mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Iringa, Wakati zozi likianza mikoa hiyo nyingine zitakuwa
zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma. Mikoa mimgine ni
Singida Tabora Geita na Kigoma.
Mkuu wa
kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit Cariah,
Akizungumza na mwandishi wetu amesema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa
ya Lindi, Mtwara, Ruvumna na Iringa wakae tayari kwani muda wowote
watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.
Pamoja na
mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248
ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa
kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa
BVR.
Dr Sisit
Ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika mashine
hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo
endeshi (Software) na upande wa Vichapishio (printer) ambazo sasa
zimetengenezewa Nchini Ufaransa umeboreshwa na nirahisi kusafishwa.(Muro)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269