MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda akiwa anafungua mkutano ulioandaliwa na mfuko wa mafao ya
kustaafu wa GEPF kwa wadau wake jijini Arusha uliolenga kujadili maswala
mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko
katika mfuko huo.
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF
Aloyce Ntukamazina akizungumza katika mkutano na wadau kutoka sekta
mbalimbali uliofanyika jijini Arusha uliolenga kujadili maswala
mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko
katika mfuko huo.
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda akiwa anasoma kipeperushi chenye maelezo kuhusu mfuko wa
GEPF,kushoto Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina,kulia ni
meneja kanda ya kaskazini Dennis Kaitwa
Kushoto Mwalimu Jonuis Lowassa kutoka idara ya utumishi wa walimu(KTSD)wilaya ya Mounduli na Longido
Afisa masoko GEPF Clement Oning’o ambaye alikuwa Mc wa shughuli hiyo akitoa utaratibu katika mkutano huo
Afisa muajiri Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Siraji Msophe akifurahia jambo katika mkutano huo
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakiwa wanateta jambo na Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina
Wadau wakiwa katika mkutano huo
Kushoto Afisa rasilimali watu na
utawala Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Isaial Bayege
akiwa ananukuu baadhi ya mambo katika mkutano huo ulioandaliwa na mfuko
wa GEPF jijini Arusha
Kulia ni Afisa Rasilimali watu katika chuo cha Nelson Mandela Bi.Honorina Mashingia
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF
Aloyce Ntukamazina akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali kuhusu mfuko wa GEPF jijini Arusha
Meneja kanda ya kaskazini kutoka mfuko wa GEPF Dennis Kaitwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni Rasmi MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.
…………………………………………….
Habari Picha na Pamela Mollel wa http://jamiiblog.co.tz
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda ameitaka mifuko ya jamii kuendelea kutoa elimu zaidi kwa
wananchi kujiunga na mifuko hiyo ili kuweka akiba ambayo itasawasaidia
kwa maisha yao ya baadaye.
Aliyasema hayo wakati
akizungumza katika mkutano wa wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika
mjini hapa uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya
kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.
Alisema kuwa, mifuko hiyo ina
manufaa makubwa sana kwa jamii hususan kipindi cha kustaafu ambacho huwa
ni kipindi kigumu sana kwa asilimia kubwa ya wastaafu ambapo wengi wao
mifuko hiyo huwasaidia sana kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.
Ntibenda alisema kuwa, kuna
idadi kubwa sana ya wastaafu ambao wangependa kujiunga na mifuko hiyo
ila kinachowawia ugumu ni kutopata elimu ya kutosha juu ya kujiunga na
mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa sana kwao.
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF
Aloyce Ntukamazina alisema kuwa ,mfuko huo umeanza kutoa elimu nchi
nzima juu ya mabadiliko ya mfuko huo ambapo wamezindua mafao mapya manne
ambayo ni fao la elimu,uzazi,fao la kuanza maisha ,na fao la kujikimu
ambapo mafao hayo yote ni yataanza kutumika katika mfuko huo hivi sasa.
Aloyce amesema kuwa,mfuko huo
wamekuwa wakijitahidi sana na kukabiliana na changamoto ya wajiri
kutofikisha mafao ya wafanyakazi kwenye mifuko kwa wakati ambapo mfuko
huo wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha makato hayo yanafika kwa wakati na
muda ulipangwa .
Aidha washiriki wa mkutano huo,
wakizungumza kwa nyakati tofauti waliutaka usimamizi wa mifuko hiyo
kuongeza mifuko zaidi ili wananchi wawe katika hali nzuri ya kiuchumi
kwa kutumia mifuko mbalimbali na kuondokana na kusongamana kwenye mifuko
michache iliyopo .
Meneja wa mfuko huo kanda ya
kaskazini ,Denis Kaitwa amesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
kubwa ya kutoa elimu kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kuwa wagumu
kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwa maisha yao.
Kaitwa alisema kuwa,kupitia
mkutano huo utawawezesha wadau hao kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi wao
na hatimaye kuweza kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wa GEPF
ambao una manufaa makubwa kwa jamii.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269