Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava
(kulia) wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach
jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la
wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi
tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto
katika utendaji kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara ya
Nishati na Madini, Marcelina Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi
Mwihava (hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE
Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini
wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani)
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
(kulia) akisoma hotuba ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa
TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini
wakiimba wimbo wa kuonyesha mshikamano ujulikanao kwa jina la “solidarity forever”
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na
Mhasibu Mkuu Mfawidhi wa Wizara ya Nishati na Madini, Michael Marandu
(kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano ili kufungua
mkutano huo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga (katikati, waliokaa
mbele) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi, Wizara
ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269