Na Masanja Mabula -Pemba .
Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imepiga marufuku uoneshaji wa video usiozingatia sheria na taratibu katika sehemu za wazi ambazo zinamkusanyika wa watu .
Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman baada ya kubaini kuwepo na watu wanaokiuka sheria makusudi na kuwataka kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria .
Akizungumza na masheha wa Wilaya ya Wete , Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa mwananchi ambaye anataka kuonyesha video anapaswa kutaka kibali kutoka taasisi zinazohusika.
Aidha amewaagiza masheha kusimamia agizo hilo kwa kuhakikisha kwamba wanaoonyesha video wanakuwa na vibali halali kisheria .
"Nawaomba
masheha mlisimamie agizo hili , hakikisheni kwamba wanaoonyesha video
katika shehia zenu wanakuwa na vibali kutoka taasisi husika " aliagiza
Mkuu wa Mkoa .
Ameeleza
kwamba vitendo hivyo mbali na kutumika kisiasa , pia vimekuwa
vikiwakosesha wanafunzi masomo yao kwani wanatumia muda wao mwingi
kuangalia video hizo.
"Serikali
ya Mkoa imebaini kwamba video hizo mbali na kutumika kisiasa lakini pia
vimekuwa ni chanzo cha wanafunzi kukosa masomo yao kwani wanatumia muda
wao mwingi kuangalia videoa badala ya masomo " alieleza .
Nao
Masheha wameahidi kulisimamia agizo kwa kutoa elimu kwa wananchi
kutambua athari za kuonyesha video bila ya kuwa na kibali kutoka taasisi
husika .
Wamekiri
kuwepo na wimbi la watu kuonyesha video hadharani bila ya kuwa na kibali
na kwamba wameahidi kutoa elimu kwa wanaohusika na uoneshaji wa video .
"Kumekuwako
na wimbi la uonyeshaji wa video katika shehia hasa nyakati za usiku ,
na wahusika hawana vibali ,kwa hili tutahakikisha kwamba tunatoa elimu
kwa wananchi kutambua athari ya kuonyesha video kinyume na sharia "
alieleza Sheha wa Shehia ya Utaani .
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba wanaoonyesha
video kwenye mikusanyiko ya watu hasa nyakati za jioni na usiku hawana
vibali jambo ambalo linaikosesha mapato serikali.(Muro)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269