Breaking News

Your Ad Spot

Apr 12, 2015

POLISI SINGIDA YAIFUNGA TIMU YA WAANDISHI WA HABARI SINGPRESS 3-2

DSC04943
Timu waandishi wa habari mkoa wa Singida iliyopambana na timu ya polisi katika mechi kali na ya kusisimua ya bonanza iliyofanyika uwanja wa Namfua.
Na Nathaniel Limu, Singida
TIMU ya soka ya jeshi la polisi mkoani Singida,imeichapa timu ya klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida goli 3-2 kwenye mchezo wa bonanza iliyoandaliwa na kufadhiliwa na kampuni ya simu Vodacom Tanzania tawi la Singida.
Mechi hiyo kali na ya kusisimua,imefanyika kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mjini hapa.
Hata hivyo,timu ya waandishi wa habari ndiyo iliyoanza kuzifumania nyavu za wapinzani wake kupitia kwa Elisha Nyamuhanga katika dakika ya 38.Elisha alifunga goli hilo baada ya kuizidi mbio ngome ya polisi na kuachia shuti kali lililomshinda kipa Luckman Omari.
Baada ya goli hilo timu ya polisi ikiongozwa na mshambuliaji wake wa kutumainiwa kamanda wa mkoa,Thobias Sedoyeka,ilishambulia mfulululizo lango la Singpress na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Damas Moris katika dakika ya 41.
Damas ambaye aling’ara kwenye mechi hiyo,aalifunga goli hilo baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kamanda Sedoyeka. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika,timu zote zilikuwa zimefungana goli 1-1.
DSC04944
Timu ya jeshi la polisi mkoani Singida,iliyopambana na timu ya waandishi wa habari mkoani Singida kwenye mechi ya bonanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua.Polisi ilishinda goli 3-2.Wa kwanza kushoto aliyesimama,ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka.
Kamanda Sedoyeka aliikosesha timu yake goli la wazi katika dakika ya 53 baada ya kupiga shuti kali lililomlenga kipa wa Singpress Ismael Abdalah.
Damas aliweza kuifungia timu yake goli zingine mbili katika dakika ya 67 na 82 wakati Singpress ilifanikiwa kuongeza goli la pili kwa Machibya Silvester katika dakika ya 71.
Wakati huo huo,timu ya polisi yab kuvuta kamba,iliweza kuigaragaraza timu ya Singpress katika mchezo huo.
Kamanda Sedoyeka aliyeratibu bonanza hilo, amewataka waandishi wa habari,askari polisi na wananchi wa mkoa wa Singida kwa ujumla,kujenga utamaduni wa kushiriki michezo,ili kuimarisha afya zao.
DSC04946
Kipa wa Singpress Ismael Abdalah,akipangua mpira ulioelekezwa golini kwake na mshambuliaji wa timu ya jeshi la polisi kwenye mechi ya bonanza iliyofanyika uwanja wa Namfua mjini hapa.
“Michezo ina faida nyingi mno, kubwa ikiwa ni kuimarisha afya,kupanua wigo wa marafiki,kujiajiri na kuajiriwa.Kwa hiyo, kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kutenga muda kwa ajili ya kushiriki michezo mbalimbali”,alifafanua.
Kamanda huyo alisema katika kipindi cha kuwepo mkoani Singida,atahakikisha bonanza zinafanyika kila mwaka ili kuimarisha mahusiano baina ya jeshi la polisi na vyombo vya habari.
DSC04949
Timu ya kuvuta kamba ya klabu ya waandishi mkoa wa Singida (Singpress), ikishiriki kuvuta kamba dhidi ya timu ya jeshi la polisi mkoa wa Singida wakati wa bonanza la michezo.Timu ya polisi iliweza kuigaragara Singpress.
DSC04939
Kamanda wa jeshi la polisi (kushoto) mkoa wa Singida,Thobias Sedoyeka, akipasha muda mfupi kabla ya kuanzwa kwa mechi ya bonanza kati ya polisi na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages