Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania, kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, imeelezea kuridhishwa kwake na namna ambavyo Mashirika ya Kimataifa naTaasisi binafsi zinavyoshirikiana na kwa karibu na serikali na taasisi zake kuimarisha sekta ya uvuvi.
Tanzania, kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, imeelezea kuridhishwa kwake na namna ambavyo Mashirika ya Kimataifa naTaasisi binafsi zinavyoshirikiana na kwa karibu na serikali na taasisi zake kuimarisha sekta ya uvuvi.
Ushirikiano huo umeifanya sekta ya uvuvi nchini kuwa wenye tija na hivyo kuchangia katika ongezeko la kupato na kuwaondoa katika umaskini jamii ya watanzania ambao maisha yao ya kila siku yanategemea sana uvuvi, na pia kuimarisha utuzaji wa mazingira ya pwani na viumbe hai.
Balozi Tuvako Manongi ameyasema hayo wakati wa mkutano wa pembezoni ( side event) uliokuwa umeandaliwa na Mpango wa Chakula Dunia ( FAO). Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano usio rasmi ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakutana ana kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya bahari na uwiano wake katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Balozi Manongi alikuwa mmoja wa wazungumzaji katika mkutano huo ambapo majadiliano yalilenga zaidi katika suala zima la uwezeshwaji wa wataalamu wa sekta ya uvuvi na wavuvi wadogo na wakati kwa kuwapatia mbinu na maarifa ya kisasa ya uvuvi endelevu na unaozigatia utuzaji wa mazingira ya bahari na viumbe hai.
Katika mchango wake, Balozi ameeleza kuwa uchumi na ustawi wa wavuvi wengi wanaoishi pembezoni mwa bahari (pwani) nchini tanzania unategemea sana shughuli za uvuvi na kutoka na ukweli huo, Serikali ya Tanzania, licha ya kukaribisha wabia katika kuiendeleza sekta ya uvivu pia inawashukuru wale wote ambao hadi sasa wametoa mchango wao wa hali na mali katika eneo hilo.
Akaongeza kuwa mafunzo na utaalamu ambao wadau hao wamekuwa wakiwapatia wataalam wa kitanzania kwa kuwashirikisha pia wavuvi ambao ndio wahusika wakuu, umesaidia sana katika kuwainua kiuchumi lakini pia kuwapatia mbinu endelevu za uvuvi na utunzaji wa mazingira.
Wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo endelevu ya sekta ya Uvuvi ikiwamo misaada ya kiufundi ni FAO na EAF- Nansen Project ya Norway.
Tanzania ni kati ya nchi 32 ambazo zinashirikiana kwa karibu na EAF –Nansen Project katika miradi mbalimbali inayohusu uwezeshwaji wa wavuvi wadogo na wakati. Aidha Tanzania ni kati ya nchi 10 za mwanzo zilizochaguliwa kutekeleza mpango huo.
Amesema Balozi Manongi, uvuvi endelevu na matumizi salama ya Bahari ni moja ya ajenda za Malengo Mpya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 (SDGs). Ajenda ambayo kwayo inasisitiza usimamizi endelevu na ulinzi wa bahari na mazingira ya pwani na viumbe hai ili kuepusha athari mbalibmali.
Vile vile ajenda hiyo ambayo ni namba 14 inasisitiza pia uwepo kwa kanuni bora zinazosimamia uvuvi ikiwa ni pamoja na kudhibiti uvuvi wa kupita kiasi na uvuvi haramu, na utoaji wa huduma za kisasa kwa wavuvi wadogo na fursa za masoko.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa ameeleza zaidi kwamba, zao la samaki pamoja na kuwa kuchanzo cha kipato kwa watanzania wengine na taifa kwa ujumla, lakini pia samaki wanachangia katika kuwapatia lishe bora watanzania na kwa sababu hiyo matumizi endelevu ya mazao ya bahari na bahari ni jambo muhimu sana.
Katika majadiliano hayo, Dr. Gabriella Bianchi ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utafiti wa samaki kutoka ofisi za FAO yeye katika mchango wake, ameelezea baadhi ya mambo ambayo wanatarajia kuyafanya katika kuzisaidia nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikiwamo na kwingineko Afrika katika masuala ya usimamizi, mafunzo na utaalamu zaidi kwenye masuala ya samaki na bahari kwa ujumla.
Akasema mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, na uchafuzi wa bahari ni baadhi ya changamoto ambazo wataalamu na watafiri wa masuala ya bahari na viumbe hai wa baharini kuamua kupanua wigo wa kazi zao za utafiti ikiwa ni pamoja na mafunzo na uwezeshaji.
Naye Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya utafiti, amesema Norway inakamilisha ujenzi wa meli mpya na ya kisasa ya masuala ya utafiti inayotarajia kuanza shughuli zake mwaka 2016.
Kwa mujibu wa Dr. Hoel meli hiyo itakuwa na vyumba vya kufundishia, maabara za picha na maabara ya tabia nchi.
--------------
PICHA ZAIDI
Balozi Manongi akibadilishna mawazo na Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni
mtaalamu wa masuala ya utaifiti na ambaye alieleza kwamba Norway iko
katika maandalizi ya mwisho ya kukamilisha meli mpya na ya kisasa zaidi
ya utafiti itakayoanza kazi mwakani.Balozi akibadilishana mawazo na Dr. Gabriella Bianchi ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya utafiti wa samaki, Dr Gabriella na Dr, Hoel wamefanya kazi kwa karibu sana na wataalamu wa Tanzania katika kuendeleza sekta ya uvuvi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa Pembezoni
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269