Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwakaribisha wageni katika hafla ya
ufunguzi wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa waajiriwa wapya Leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo
akimkaribisha Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo na kuwataka washiriki
kushiriki kikamilifu kwenye kipindi cha mafunzo ili waweze kuwa na mbinu
thabiti za ukusanyaji kodi kwa maslahi ya Taifa.
Naibu Mkurugenzi kitengo cha Rasilimali Watu Bw. Victor
Kimaro akiwaeleza washiriki wa Mafunzo namna mchakato ulivyofanyika na kuwataka
kuthibitisha ubora wao katika kipindi chote cha mafunzo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Bw. Rished
BADE akiongea na washiriki wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi na kuwataka kufanya
kazi kama watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kutumia fursa hiyo
kujiimarisha kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi
inayohitaji uadilifu na ueledi wa hali ya juu katika kuitekeleza, wakati wa
hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo
wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo
hayo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala
utakaotumia katika mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya
Jairo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya
washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushoto ni Mkuu
wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya
washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa pili kushoto ni Mkuu
wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Rished Bade(wa sita kutoka Kulia) na Mkuu wa Chuo cha uongozi
wa Kodi Prof. Isaya Jairo (ITA) (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa
katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo baada ya kuyazindua leo
Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269