(PICHA NA JOHN LUKUWI).
Baadhi
ya wanafunzi na walimu kutoka Shule 11 za Sekondari katika Wilaya ya
Temeke wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Afisa Elimu-Sekondari wa
Wilaya ya Temeke Ndugu Donald Chavila (hayuko pichani) wakati alipokuwa
akifungua rasmi semina ya siku tano inayozungumzia uzuiaji wa mimba za
utotoni kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo tarehe 13.4.2015 kwenye ukumbi wa
sherehe wa Kibasila Sekondari.
Afisa Elimu-Sekondari wa Wilaya ya Temeke Bwana Donald Chavila
akifungua rasmi semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa
wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke. Semina hiyo
inaendeshwa na Taasisi ya WAMA, ikishirikiana na Shirika la Engender
Health la Marekani na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Serikali ya
Marekani,USAID. Baadhi
ya wanafunzi na walimu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Temeke
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Afisa Elimu-Sekondari wa
Wilaya ya Temeke Ndugu Donald Chavila wakati akifungua semina hiyo
inayofanyika Kibasila Sekondari. Baadhi
ya wanafunzi kutoka Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke
wakisikiliza kwa maini baadhi ya mada zilizokuwa zikitolewa wakata wa
semina ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika
wilaya hiyo. Semina hiyo ya siku 5 inafanyika Kibasila Sekondari na
ilifunguliwa rasmi tarehe 13.4.2015. Washiriki
wa semina wakiwa wamegawanyika katika vikundi mbalimbali ili kujadili
mojawapo ya mada iliyokuwa imetolewa na baadaye kila kundi kuwasilisha
kwenye semina hiyo. Washiriki
wa semina wakiwa wamegawanyika katika vikundi mbalimbali ili kujadili
mojawapo ya mada iliyokuwa imetolewa na baadaye kila kundi kuwasilisha
kwenye semina hiyo. Mwanafunzi
mshiriki wa semina ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za
sekondari katika Wilaya ya Temeke akiwasilisha majibu ya majadiliano ya
kikundi chao katika siku ya kwanza ya semina hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269