Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2015

TAWLA WAZINDUA MAADHIMISHO YAKE YA KUTIMIZA MIAKA 25

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chama cha Wanawake Wanasheria  Tanzania (TAWLA),  Margareth Ringo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa, katika  maadhimisho ya miaka 25 ya kujengea uwezo na kufanya uchechemuzi juu ya haki ya wanawake. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile na Mjumbe wa Baraza la TAWLA, Annmarie Mavenjina.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile (kulia), akizungumza katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Mweka Hazina wa TAWLA, Asina Omari, Mjumbe wa Baraza la TAWLA, Annmarie Mavenjina na  Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chama cha Wanawake Wanasheria  Tanzania (TAWLA),  Margareth Ringo.
 Mkutano ukiendelea.
 Maofisa wa TAWLA wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Mratibu wa maswala ya Wanachama wa TAWLA, Josephiner Arnold (kushoto), akumuelekeza jambo Ofisa Habari wa TAWLA, Goodness Mrema wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Ukumbi wa YWCA Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
 Wanahabari wakichukua taarifa ya maadhimisho hayo.
  Wanahabari wakichukua taarifa ya maadhimisho hayo.
Wanahabari wakichukua taarifa ya maadhimisho hayo.

Dotto Mwaibale
CHAMA cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwa kipindi cha miaka 25 kimetoa msaada wa kisheria kwa wanawake milioni tano katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Dodoma.

Hayo yalielezwa na Makamu Mwenyekiti wa Balaza la TAWLA, Margareth Ringo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika maadhimisho ya miaka 25 ya kujengea uwezo na kufanya uchechemuzi juu ya haki ya wanawake.

"TAWLA inajivunia mafanikio makubwa iliyopata ndani ya kipindi cha miaka 25 kimeweza kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake wasiopungua milioni tano kupitia vituo vilivyopo Dar  es Salaam, Tanga,Arusha na Dodoma" alisema Ringo.

Alisema pia wameweza kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa kutumia simu bila malipo kupitia namba 08007510101/0800110017.

Ringo aliongeza kuwa katika kuhakikisha jamii za pembezoni zinaweza kuifikia haki TAWLA imetoa mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria 402 katika wilaya 18 Tanzania ambazo ni Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Chamwino, Mpanda vijijini, Mpanda Mjini, Arumeru, Longido, Monduli, Arusha, Karatu, Muheza, Tanga, Kisarawe, Mvomero, Ilemela Magu na Ilala.

Alisema wasaidizi hao wamesaidia kuwafikia zaidi ya watu 10,500 waliokuwa na matatizo ya kisheria na pia namba kubwa zaidi wameweza kupata elimu ya maswala ya kisheria.

Aliongeza kuwa pamoja na kutoa msaada wa kisheri  wameweza kuihamasisha jamii juu ya masuala ya kisheria kupitia machapisho mbalimbali na vyombo vya habari na michezo ya kuigiza ambapo watu zaidi ya milioni 15 wamefikiwa.

Alisema chama hicho kimekuwa kikishiriki kutetea mabadiliko ya sheria kandamizi kwa wanawake na za kuwalinda, mchakato wa kupitisha kwa sheria ya mtoto na sheria ya makosa ya kujamiana, kuchangia uteuzi na ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi na kuwa chama hicho kina mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wakiwemo asasi zisizo za kiserikali, serikali kuu na za mitaa.

Ringo alisema katika kusherehekea mafanikio ya miaka 25 TAWLA kuanzia Mei 10 hadi 29 wanatakuwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji wa kuandika wosia na utaenda pamoja na uandikishaji wosia bila gharama kwa wale ambao watakuwa tayari katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Dodoma pamoja na kutoa msaada wa kisheria katika baadhi ya mikoa. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habari za jamii.com/)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages