Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) na ujumbe wake wakipewa maelezo na Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya cha Wurzburg Nchini Ujerumani katika ziara ya kikazi .
[Picha zote na Ramadhan Othman,]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo
kutoka kwa Mkuu wa Idara ya maradhi ya Tropic Prof.Dr.med,August Stich
wakati alipotembelea katika Chuo cha Afya kinachotoa huduma ya matibabu
kujishuhulisha na tafiti mbali mbali za maradhi ya Binadamu akikwa
katika ziara ya kikazi katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani Chuo
hicho kimetoa mchango mkubwa katika kupambana na maradhi ya Ebola
yaliyotokea katika Nchi za Magharibi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein (kushoto) akiwa katika chakula maalum kwa ujumbe wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein wakati ujumbe huo ukiwa katika ziara ya kikazi katika Mji wa
Wurzburg uliposhiriki katikaTamasha la Maonesho ya Muziki na Utamaduni
liliofanyika na kujumuisha Wasanii na Wanamuziki mbali mbali Afrika na
Nchi nyengine Duniani ikiwemo Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi
wengine akiwepo mwenyeji wake Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg
Mhe,Christian Schuehadt (kulia) katika chakula cha jioni
kilichoandaliwa kwa heshma yake akiwa katika ziara ya kikazi katika Mji
wa Wurzburg Nchini Ujerumani alipohudhuria katika Tamasha la 27 la
Muziki na Utamaduni lililoshirikisha Wasanii mbali mbali na Wanamuziki
wakiwemo wa Nchi za Afrika na Duniani kwa ujumla,
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Mshauri wa
Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa
(kushoto) na Msaidizi Naibu Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg Dr.Adolf
Bauer wakati wa chakula maalum cha jioni kilichoandaliwa kwa Ujumbe wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani katika Mji wa Wurzburg
alipohudhuria katika Tamasha la 27 la Muziki.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269