Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya
Kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) Bi. Johari Kachwamba akiwaelimisha
Viongozi wa Kata ya Mwasanga na Tembela kuhusu majukumu ya TGDC leo 7
Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
Mhandisi Mwandamizi toka Wizara
ya Nishati na Madini, Bwana. Jacob Mayalla akiwaelimisha Viongozi wa
Kata ya Mwasanga na Tembela kuhusu historia ya tafiti za jotoardhi kwa
mkoa wa Mbeya leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
Baadhi ya Viongozi wa Kata
ya Mwasanga na Tembela wakifuatilia kwa makini elimu ikiyotolewa na
Wayendaji wa TGDC leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
………………………………………………………………………………………………………..
NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, MBEYA.
Nishati ya jotoardhi imeelezwa
kuwa ni nishati usiyokuwa na kikomo kwani pindi inapovunwa huwa haiishi
na matumizi yake yanakuwa endelevu kwasababu pindi mvuke unapopatikana
toka katika maji ya jotoardhi, maji yake hutumiwa kwa shughuli za moja
kwa moja ikiwemo ukaishaji wa mazao, uzalishaji samaki ikiwemo na
utalii.
Hayo yameelezwa leo na Mhandisi
Mwandamizi toka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana Jacob Mayalla wakati
Timu ya Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC)
ikiendelea na kampeni yake ya kuelimisha viongozi pamoja na wanavijiji
kuhusu faida ya jotoardhi nchini.
Mayalla amesema kuwa utafiti
kuhusu upatikanaji wa jotoardhi ulianza miaka ya nyuma ya 1976 hadi 1978
ambapo mkoa wa Mbeya umekuwa miongoni mwa mikoa ambayo jotoardhi
inasemekana ipo kutokana na tafiti hizo.
“Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa
mikoa iliyobarikiwa kuwa na jotoardhi, hivyo Serikali kupitia Kampuni
hii ya TGDC inakusudia kuanza shughuli za upimaji ili kuweza kupata
nishati hii na kuweza kutatua changamoto za upatikanaji wa umeme katika
mkoa huu”, alisema Mayalla.
Akitaja baadhi ya matumizi ya
moja kwa moja, Mhandisi Mipango toka TGDC, Bwana Chagaka Kalimbia
ameeleza kuwa, jotoardhi ina matumizi mbalimbali ikiwemo kupadha nyumba
joto, kuzalisha mazao ya mbogamboga kwa kutumia Vitalu Nyumba, vyanzo
vya kitalii kwa nchi pamoja na matumixi mengineyo ambayo yanapelekea
kuongeza vipato vya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Mradi huu una manufaa kwa
wananchi kwa mfano kwa mkoa wa Mbeya ambao kuna baridi kali, jotoardhi
inaweza kutatua changamoto hii kwa kutengeneza miundombinu ambayo
itasaidia kupasha nyumba joto, lakini pia kwasababu mkoa huu unategemea
kilimo, basi jotoardhi hii itakuwa mkombozi kwa uzalishaji mkubwa wa
mazao mbalimbalu kwa kukaushia maxso yao kwani nishati ya jua katika
maeneo haya siyo ya uhakika”.
Naye Afisa Mawasiliano wa TGDC,
Bi. Johari Kachwamba ameeleza mandhari nzima wa madhumuni ya TGDC kwa
wananchi na kwa Taifa zima ikiwemo hali ya uzalishaji wa umeme hapa
nchini, historia ya TGDC, Dira na dhamira kuu ya TGDC ili kuifanya jamii
ipate uelewa mzuri kuhusu majukumu ya Kampuni hiyo.
Kwa upande wake Afisa Sayansi
ya Jamii, Bi. Eva Nyantori ameeleza masuala mbalimbali kuhusu namna gani
jamii inashitikishwa na mradi huo kwa manufaa ya wananchi hususani
fursa mbalimbali ambazo jamii inatarajiwa kuzipata zikiwemo fursa za
ajira ambazo huleta kipato hali ambayo inapelekea uchumi wa eneo kukua
kwa kasi kutokana na na nishati hiyo.
“Jamii itarajie kupata fursa
mbalimbali mfano sekta za barabara, ajira kwa wananchi, kodi itokanayo
na mradi huo, upatikanaji wa umeme wa nafuu kwa wakazi wa eneo husika,
hivyo ni matumaini yetu kuwa nishati hii itapunguza gharama kwa wananchi
wa mkoa huu”, alisema Nyantori.
Akizitaja changamoto za mradi
huo, amesema kuwa kuna Sheria namba 4 na 5 ya 1999 ili kuweza kufanya
fidia kwa maeneo yayaksyohusika na mradi ambapo Sheria hiyo inaitaka
kufanya fidia hiyo ndani ya miezi Sita kabla ya mradi huo kuanza rasmi
kuchimbwa, lakini elimu kuhusu fidia hiyo itatolewa ili kumfanya
mwananchi apate kuelewa.
TGDC inatarajia kuzalisha zaidi
ya Megawati 200 za nishati ya umeme kwa mkoa wa Mbeya ambao utatokana
na nishati ya jotoardhi ambapo kwa sasa mkoa huo unatumia Megawati 40.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269