Breaking News

Your Ad Spot

Aug 9, 2015

SIMBA YASHUSHA SILAHA KALI

KOCHA wa Simba, Dylan Kerr
KOCHA wa Simba, Dylan Kerr ameanza kupagawa na kiwango cha timu yake na amewataja mabeki wake wa pembeni Hassan Kessy na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kama silaha zake mbili za kupandisha mashambulizi.
Wakati Kerr akijinadi na mabeki, kipa Luis Rideiro, Mbrazili aliyekuwa akicheza Ureno katika klabu ya Sporting B leo Jumamosi anatarajia kutua Dar es Salaam kwa ajili ya kuichezea Simba.
Wakati Mbrazili huyo akitarajiwa kutua leo, jana Ijumaa, straika Mrundi, Kevin Ngaisenga wa klabu ya AO Bujumbura alitua Dar na kujiunga na timu hiyo.
Keshokutwa Jumatatu, beki kutoka Mali, Makani Dembele anataraji kufanya majaribio.(P.T)
Dembele amewahi kuichezea JS Kabliye ya Algeria.
Habari hizo zilithibitishwa na Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye alisema klabu yake ina uhakika wa kumsajili kipa na mshambuliaji kutokana namahitaji ya kocha wao wakati suala la beki litakuja baada ya kuangalia uwezo wake.
Kwa upande wake Kerr alisema Kessy, na Tshabalala wana vigezo vyote vinavyohitajika kwa mabeki wa pembeni na kasi yao uwanjani inavutia muda wote jambo linaloiwezesha timu kucheza anavyohitaji.
Kerr pia alisema safu yake ya ulinzi ya pembeni imekamilika kutokana na uwepo wa Mrundi Emiry Nibomana na Samir Haji Nuhu ambao pia wameonyesha uwezo wa kuvutia mpaka sasa.
“Unapokuwa kocha halafu una wachezaji wazuri lazima uwe na furaha, kuna baadhi ya maeneo ambayo yanavutia katika timu,” alisema.
“Uwepo wa Kessy na Tshabalala ni silaha kubwa kwangu, wanapanda kadri wanavyojisikia na hawaachi nafasi nyuma, timu ikipoteza mpira wanarudi haraka.
APATA TABU
Simba leo itacheza na SC Villa ya Uganda katika maadhimisho ya Simba Day na Kerr amebainisha kuwa kazi kubwa kwake katika pambano hilo ni kuchagua kikosi kitakachoanza kwa kuwa wachezaji wake walionyesha uwezo Zanzibar.
Katika mechi na Villa huenda Mbrazil akapata nafasi ya kucheza pamoja na straika Mrundi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages