Breaking News

Your Ad Spot

Sep 24, 2015

BARCA YATULIZWA LA LIGA, YAPOKEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI

Messi vs Celta Vigo
Barcelona wamechpwa bao 4-1 na Celta Vigo kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye mechi za ligi ya Hispania marufu kama La Liga mchezo uliochezwa Jumatano usiku.
Nalito alianza kuifunga timu yake ya zamani na kuipa Celta Vigo bao la kuongoza huku akimtengenezea Iago Aspas mabao mengine mawili kwenye mchezo ambao safu ya ulinzi ya Barcelona inayoongozwa na Gerard Pique ikionekana kuyumba.
Shuti la Lionel Messi liligonga mwamba mapema mwa kipindi cha pili huku mlinda mlango wa Celta Vigo Sergio Alvarez akiokoa michomo kadhaa kabla hajafungwa na Neymar wakati wenyeji Celta wakikamilisha ushindi wao wa goli 4-1 kwa goli la dakika za lala salama lililofungwa na John Guidetti aliyeingia akitokea benchi.
Ushindi huo kwa Celta unawafanya wafikishe pointi 13 kwa mechi tano ambazo wamecheza hadi sasa katika msimu huu wakati kichapo hicho kwa upande wa Barcelona kinakuwa ni cha kwanza kufuatia kuanza ligi vyema kwa ushindi wa michezo minne iliyopita.
Celta walianza vyema mchezo huo lakini Barcelona walitengeneza nafasi dakiza za mwazo za kipindi cha kwanza. Iniesta alikimbia na mpira kabla ya kumuwekea Messi pasi murua lakini shuti lake liliokolewa na golikipa wa Celta Sergio Alvarez.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages