Breaking News

Your Ad Spot

Sep 29, 2015

DK MAGUFULI ANG'ARA DODOMA, AAHIDI KUWAPATIA VIJANA WANAOMALIZA VYUO VIKUU MIKOPO YA KUANZISHIA KAMPUNI

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Pagawa, Jimbo la Ismani, Iringa Vijijini

Akihutubia Kwa nyakati toifauti katika kampeni alizozifanya leo katika majimbo ya Ismani, Iringa na Kibakwe na Mtera , ameahidi akishinda ataanzisha mpango maalumu wa kuwakopesha vijana wanaomaliza vyuo vikuu ili waanzishe kampuni mbalimbali zikiwemo za ujenzi wa majengo na barabara ili kupunguza tatizo la ajira nchini

.Tayari Dk Magufuli amefanya kampeni katika mikoa 18 bado 13 ambapo ametumia usafiri wa barabara kwa jumla ya Km 17,500.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (kushoto) na mgombea ubunge Jimbo la Mtera, Livingstone  Lusinde pamoja na baadhi ya wagombea udiwani kupitia chama hicho wakiwapungia mikono wananchi walipokuwa wakijinadi katika mkutano wa kampeni jimboni Mtera, Dodoma
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwaomba kura katika mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa, Dodoma
 Mgombea ubunge Jimbo la Isimani, William Lukuvi akijiadi kwa wanancho pamoja na kumuombea kura Dk Magufuli katika Kata ya Pagawa, Iringa Vijijini
 Dk Magufuli akiwapungia wananchi kwa kofia aina ya pama katika Kata ya Pagawa

 Wananchi wakimshangilia kwa nguvu Dk Magufuli alipowasili kwenye mkutanoi wa kampeni katika Kata ya Migoli Jimbo la Ismani, mkoani Iringa

 Mke wa Mgombea ubunge Jimbo la Ismani, William Lukuvi, Germania Lukuvi akimuombea kura kwa wananchi mumewe na Mgombea urais, Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni Kata ya Migoli, Iringa Vijijini leo.
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwaomba kura katika mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa, Dodoma
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa, Dodoma, George Simbachawene wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo
 Wananchi akishangilia baada wakati mgombea ubunge Jimbo la Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde, akijinadi jukwaani ambapo pia aliwananga  Mgombea urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa  na anayemkampenia, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kuwa tabia zao ni sawa na Popo anayejinyea. Wa pili kulia ni Mwernyekiti wa CCM wa Wilaya ya Chamwino,
 Dk Magufuli akimpongeza Lusinde kwa hotuba yake nzuri
 Lusinde akipongezwa na John Malecela kwa kumfanyia kampeni nzuri Dk Magufuli. Lusinde pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM.
 Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela akifurahi alipokuwa akipanda jukwaani kuwapigia kampeni Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli na Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde katika mkutano wa kampeni Jimboni Mtera, Dodoma
 Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela akihutubia alipokuwa akiwapigia kampeni Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli na Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde katika mkutano wa kampeni Jimboni Mtera, Dodoma
 Dk Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa wakifurahia jambo wakati wa mkutano wa kampeni jimboni Mtera, katika Mji wa Mvumi Mission leo.
 Sehemu ya umati wa wananchi ukinyoosha mikono juu kukubali kumpigia kura Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli katika mkutano wa kampeni Jimboni Mtera, Dodoma
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Mvumi Mission, Jimbo la Mtera
 Dk Magufuli akimnadi Livingston Lusinde anayegombea ubunge Jimbo la Mtera
 Dk Magufuli akimshukuru John Malecela kwa kumfanyia kampeni katika Mji wa Mvumi Mission, Jimbo la Mtera leo
Dk Magufuli, Malecela, Lusinde na Kimbisa wakipiga makofi walipokuwa wakiondoka baada ya mkutano wa kampeni kumalizika katika Mji wa Mvumi Mission, Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages