Rais Putin amekuwa rafiki mkubwa wa Rais Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad amefanya mashauriano na Rais wa Urusi Vladimir Putin baada yake kufanya ziara ya kushtukiza Moscow.
Msemaji wa Rais wa Urusi Dmitry Peskov amesema Assad "alikuwa kwenye ziara ya kikazi Moscow" Jumanne na alifanya mazungumzo na Bw Putin.
Mwishoni mwa mwezi jana, ndege za kijeshi za Urusi zilianza kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na wapinzani wa Assad nchini Syria.
Urusi imejitetea na kusema inashambulia tu makundi ya kigaidi na wapiganaji wa Islamic State.
Bw Peskov ameambia wanahabari kwamba viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu viva hivyo alivyosema ni dhidi ya magaidi.
Aidha, walizungumzia kuendelea kwa mashambulio ya ndege za Urusi na mpango wa Syria kuhusu wanajeshi. Haijabainika iwapo Bw Assad bado yuko Moscow au amerejea Damascus.
Hiyo ndiyo ziara ya kwanza kabisa kufanywa na Bw Assad nje ya nchi tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria 2011, runinga ya serikali nchini Syria imesema.
Taarifa kuhusu mazungumzo hayo iliyotolewa na Kremlin inaonyesha Bw Putin akieleza Syria kama “rafiki” na kusema Urusi iko tayari kuchangia “sio tu kijeshi...bali pia katika mchakato wa kisiasa” kurejesha Amani nchini humo.BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269