CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi
kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka
unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya
wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura.
Ujumbe huo unaokwenda kwa
watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu
kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa
husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili
aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais.
Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu
za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale
baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na
mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais.
Ukiacha utaratibu wa kampeni za
moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua
ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi
utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na
ushindani mkubwa.
Pengine hili ndio bao la mkono
lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani
wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi.
Kutokana na hatua hiyo ina maana
kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura
mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua
katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa
hili.
Chama cha Mapinduzi CCM
kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa
kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269