Rais Jakaya Kikwete
akimpongeza kwa furaha, Ikulu jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva kumtangaza
Dk. Magufuli kuwa mshindi, alipotangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofayika Oktoba 25, mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimsomea sms za pongezi kutoka kila pembe ya dunia mshindi wa
kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akipokea salamu za pongezi kutoka kwa aliyekuwa mgombea Urais kwa
tiketi ya ACT Wazlendo, Mama Anna Mghwira, baada ya Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kumtangaza kuwa mshindi, wakati akitangaza rasmi matokeo
ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako yeye na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja
kupitia vituo vya televisheni. Dkt Magufuli amemshukur sana Mama Mghwira
na kumwita mkomavu wa siasa na mwana-Demokrasia wa mfano jioni hii
Mama Salma Kikwete akimpongeza
mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt
John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tais kutangaza
matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia
kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya
televisheni
jioni hii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea kwa furaha mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya
CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza
rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako
walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo
vya televisheni jioni hii (Picha zote na IKULU)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269