Leo
Jumtano, 21.Oktoba 2015. Ni siku muhimu sana ya kuzaliwa mdau
mwanahabari na blogger Andrew Ramadhan Chale (pichani). Tunamuombea kila
la heri, Afya njema na maisha marefu na kazi yenye furaha katika
kuhabarisha jamii kupitia blog.
Alizaliwa
siku kama ya leo 21 Oktoba, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga, Ilala
Jijini Dar es Salaam-Tanzania. Anabainisha kuwa, kufikisha miaka 30,
leo hii ni jambo la kujivunia kwani amepitia changamoto nyingi za maisha
hivyo anamshukuru kila mmoja aliyegusa maisha yake.
Pia
mdau anawakaribisha kuungana nae katika tukio maalum la kujumuika
pamoja na watoto wa kituo cha Tumaini la Maisha, wanaoapatiwa matibabu
ya matatizo ya ugonjwa wa Kansa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Tukio
hilo litafanyika kuanzia mchana wa saa nane na kuendelea hadi saa 11,
jioni, kutakuwa na utoaji wa zawadi, kufanya shughuli za kijamii za
kujitolea na kubadilishana mawazo na watoto/ wazazi na walezi wa watoto
hao. Katika eneo la hostel hizo zilizopo ndani ya Hospitali ya
Muhimbili.
Kwa wanaoweza kujumuika nae wasiliana nae kupitia Whatsapp 0767076376 ama mpigie 0719076376
wadau mnaweza kuungana kwenye mitandao ya kijanaa kupitia facebook:https://www.facebook.com/anderew.chale
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269