Majeshi
ya Kenya yawaua Al Shaabab 15Jeshi la Kenya limewauwa wapiganaji 15 wa
al shabaab katika makabiliano ya hivi punde zaidi.
Majeshi ya Kenya ambayo yako chini ya muungano wa Afrika AMISON, yalishambulia kambi ya Al shabaab Kusini mwa Somalia.
Kwa
mujibu wa msemaji wa jeshi la Kenya kanali David Obonyo '' jeshi hilo la
Kenya lilikabiliana na wapiganaji wa Al shabaab katika kambi ya
wapiganaji hao ya Yantoi karibu na mto Juba na kuweza kuwauwa wapiganaji
wa Alshabaab kumi na watano.''
''Makabiliano hayo yalitokea mwendo wa saa kumi na moja Alfajiri''
AMISON
lilitekeleza shambulizi hilo chini ya operesheni mahsusi ya Juba
Corridor ambalo lengo lake ni kuwatimua wapiganaji wa Al shabaab kutoka
maeneo hayo.
Wanamgambo
wa al shabaab, wameishambulia Kenya mara kadhaa;wanapinga kuwepo kwa
majeshi ya Kenya nchini humo.Miezi miwili iliyopita, jeshi la muungano
wa AMISON lidhibiti mji wa Baardhere uliyopo katika bonde la Juba .
Aidha wametwaa makao makuu ya kundi hilo la Al shabaab ya Dinsor Kusini mwa Somalia.
Tangu
hatua ya majeshi ya Kenya yaingie Somalia kupigana na wanamgambo wa al
shabaab , Kenya imeshabuliwa mara kadhaa na wapiganaji hao ambao
wanapinga kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini humo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269