Breaking News

Your Ad Spot

Oct 21, 2015

MAMA SAMIA AKUTANA NA WANAWAKE WA UWT, WALEMAVU NA WAJASIRIAMALI MKOA WA DAR ES SALAAM KUJUA CHANGAMOTO ZAO

 Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais kupitia  Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kushoto), akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), baada ya kupokea changamoto zao Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.

 Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba akizungumza katika mkutano huo.
 Mmoja wa viongozi kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), Nasria Nasri (kushoto), akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
 Mhasibu wa Kitengo cha Fedha, Magogoni, Charles Temba akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto mbalimbali ambapo alimuomba mama Samia, watu wenye ulemavu watengewe luzuku.
 Mwakilishi wa Walemavu, Kuruthum Dindili akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
 Musa Hassan akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
 Mwakilishi wa Wajasiriamali kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Siriel Mchemba akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto walizonazo.
 Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais kupitia  Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kushoto), akipunga mkono kuwasalimia wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), wakati akiingia ukumbini kwenye mkutano wa kupokea changamoto zao Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba

Wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), wakiwa kwenye mkutano huo.


 Wakina mama wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.

Mwanamuziki, Khadija Shabani 'Keisha' akiimba wimbo maalumu wa kampeni katika mkutano wa Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais kupitia  Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan  uliowakutanisha wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), baada ya kupokea changamoto zao Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam
Mmoja wa wanashirikisho la walemavu akishangilia jambo.



Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA Mwenza wa Chama cha Mapinduzi Samia Suluhu Hassan amewaahidi  watu wenye ulemavu kuwa atashirikaina nao katika changamoto zao zinazowakumba.

Akizungumza Dar es Salaam leo katika mkutano uliwakutanisha Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Shirikisho la walemavu (Shivyata), Samia alisema atawasaidia walemavu kwa uwezo wao na si kwa ulemavu wao.

"Katika serikali yangu nitahakikisha kuwa tunawasaidia walemavu kwa uwezo wao na sio kwa ulemabvu wao kwani walemavu wanao uwezo wa kufanya chochote kama watu wengine,"alisema.

Alisema katika kuwasaidia walemavu hao ni lazima kuwaandalia mazingira ya miundombinu iliyo bora mitaji ya kuwakwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Pia alisema katika serikali yake kutatengwa maeneo maalum kwa ajili wafanyabiashara na masoko matatu kwa jiji la Dar es Salaam yaani katika wilaya ya Ilala,Temeke na Kinondoni.

"Tutaiyomba Halmashauri za manispaa kutengwa maeneo maalum maalum kwa ajili ya wafanya biashara ndogondogo   pamoja na kuiwepo na mamlaka maalum ambayo itashghulika na sekta hiyo isiyo rasmi kwani kwa sasa halmashauri zinawatoza kodi kwa kuamua wenyewe,"alisema.

Alima katika harakati hizo kutaingwa taasisi ambayo itatengewa sh.bilioni 10 ambayo itawafanya nma kuunganishwa katika mfuko wa hifadi za jamii na itasimamiwa kwa uimara wa hali ya juu.

Akiwazungumzia wananchi wa vijijini Suluhu alisema katika srikali yake kutatengwa milioki 50 kwa kila kijiji  lengo likiwa kuwapatia maendeleo  na kukopeshwa kwa ajili maendeleo.

Kwa upande mwingine Suluhu aliwazungumzia  wazee na kusema hasa wale wazee ambao hawajaajiriwa na serikali kwa kuandaa taasisi ambayo itakuwa inawashughulikia wazee.

"Tutapitisha sensa ya wazee na kuweza kufahamu wazee wako wangapi ili kuweza kuwasaidia na kuwapa mafao ambayo itawasiadia kwa kiasi kikubwa,"alisema.

"Awamu ya tano tumejipanga kwani hapa ni kazi tu,tukopesheni kura na sisi tutawalipa masendeleo pamoja na kututafutia kura katika kila eneo,"alisema.

Kabla Mgombea huyo hajaanza kuongea mmoja wa majsiramali alisema Siriel Mchembe alimweleza mgombea huyo kuwa wanahitaji maeneo ambayo itakuwa hawafukuzwi na migambo.

Aidha mmoja wa walemavu kutoka katika kijiji cha feri Charles Temba alisema wanahitaji sehemu ambayo ya kupaki bajaji zao kutokana na magari ya mwendo kasi kuanza.

Kwa upande mwingine mlemavu wa ngozi Mussa Hassan alimwambia mgombea huyo kuwa iwe mstari wa mbele kuwatetea walemavu wa ngozi hasa katika masuala kuuliwa kisa tu ni walemavu.  

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages