11.00am:Mgombea wa urais kupitia chama cha CHADEMA Edward Lowassa atarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari mda wowote kuanzia sasa
10.30am:Chama cha ACT Zanzibar
Chama
cha Uzalendo cha ACT kisiwani Zanzibar kimeiandikia barua tume ya
uchaguzi kisiwani humo ZEC kikiitaka kutoa matokjo ya uchaguzi kwa
haraka.Chama hicho kupitia naibu wake Ali Makame kinasema kuwa
kutotolewa kwa matokeo hayo kunaathiri huduma kwa wananchi.
10.00am:Vichwa vya habari vinavyogonga magazetini nchini Tanzania.
9.30am:Chama
cha CCM kinachoongozwa na mgombea wa urais John Magufuli kimeshinda
majimbo yote ya ubunge katika eneo la Dodoma huku muungano wa Ukawa
chini ya uongozi wa Edward Lowassa ukichukua viti vingi katika mji wa
Dar es Salaam.
9.00am:NEC yatoa ufafanuzi kuhusu matokeo
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Damian Lubuva ametoa
ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya rais kutoka majimbo
mbalimbali akisema kuwa tume hiyo inatoa matokeo hayo kutoka kwa
wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo yote nchini..Ameongezea kwamba
hakuna mgombea wala chama kinachopendelewa katika suala la kutangazwa
kwa matokeo na kwamba mshindi atapatikana tu kupitia kura nyingi.
7.00am:Washerehekea Kinondoni
Kulikuwa na sherehe katika jimbo la Kinondoni nchini Tanzania baada ya chama cha CUF kushinda katika eneo hilo.
Vijana waliokuwa wakifurahia ushindi huo waliimba na kuzunguka na bajaji wakiusifu ushindi huo na chama chao.
Hatahivyo maafisa wa polisi katika eneo hilo walifika katika eneo hilo na kuhakikisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea.
6.00am:Hali ya wasiwasi yatanda Zanzibar
Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.
Vyombo
vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya
sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza
kuwa mshindi.
Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha
CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi
yake.
UMEAMKAJE?
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini
Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu
matukio tofauti nchini humo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi jana ilitangaza
matokeo ya majimbo takriban 100 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo.
Tunafuatilia pia hali ilivyo Zanzibar baada ya
mtafaruku jana kuhusu kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi. Wakati mmoja
maafisa wa usalama walizingira kituo kinachotumiwa na Tume ya Uchaguzi
Zanzibar kutangaza matokeo na hakuna aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka.
Tume ya uchaguzi humo visiwani kufikia jana jioni ilikuwa imetoa matokeo
ya
majimbo 31 kati ya majimbo yote 54.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269