Msanii
aliyeshiriki katika msimu wa tatu wa Coke Studio unaoendelea kuoneshwa
Clouds TV Vanessa Mdee, amepongezwa kwa kupata tuzo ya msanii bora wa
kike Afrika Mashariki kwenye tuzo za Afrimma zilizofanyika Marekani hivi
karibuni.
Pongezi
hizo zimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo inaendesha onyesho la
kusisimua ya muziki la Coke Studio ambalo linaendelea nchini kupitia
luninga ya Clouds na kuwavutia watazamaji wengi wa muziki nchini ikiwemo
nchi nyingine za Africa.
Meneja wa
Biashara za Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka amesema kuwa wanajivunia
kuona mshiriki wa Coke Studio mwaka huu anazidi kupata mafanikio kwa
kushinda tuzo nyingine zaidi.
“Mafanikio
ya Vanessa yametufurahisha sana akiwa ni mmoja wa wasanii wa Coke
Studio mwaka huu tuna imani naye kubwa kuwa ataendeleza kipaji chake cha
muziki na kuweza kupata mafanikio zaidi.
Wasanii
wanne kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka
huu ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na
mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, Fid Q
amefanya bonge la kolabo (mash-up) na Maurice Kirya kutokana Uganda,
Gwiji wa Bongo fleva nchini Ali Kiba amefanya kolabo matata(mash-up) na
Victoria Kimani kutoka nchini Kenya na wakati Vanessa Mdee amefanya
kolabo matata(mash-up) na mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria
ajulikanaye kama 2Face.
Wanamuziki
wengine wa Tanzania walioshinda tuzo za Afrimma ni Diamond Platnumz
ambaye alifanikiwa kukomba tuzo 3 ambazo ni Video bora ya kucheza NANA,
Msanii bora wa Afrika Mashariki na msanii wa mwaka, Diamond pia
alishiriki kwenye msimu wa pili wa Coke Studio mwaka jana.
Ommy Dimpoz naye alijishindia tuzo ya msanii bora anayechipukia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269