Ndugu zangu,
Hii ni
nchi yetu tuliyozaliwa. Ni nchi tunayoipenda sana. Tunashiriki leo, kama
taifa moja, kulijenga daraja muhimu litakalounganisha
Jana na Kesho yetu. Hakuna mmoja wetu atakayeachwa nyuma, ni daraja tutakalovuka wote katika furaha na huzuni.
Jana na Kesho yetu. Hakuna mmoja wetu atakayeachwa nyuma, ni daraja tutakalovuka wote katika furaha na huzuni.
Kama
taifa, Watanzania hatujawahi kushindwa mapambano yoyote tuliyoshiriki.
Mara zote, siri kubwa ya ushindi wetu ni Umoja Wetu wa Kitaifa. Misingi
ya mradi wa ujenzi wa Umoja wa Kitaifa iliwekwa na Mwalimu Nyerere na
wenzake.
Uchaguzi
huu usiwe chanzo cha kuibomoa misingi hiyo. Jana jioni nikiwa hapa
Iringa nilifurahishwa sana kuwaona wafuasi wa Chadema na CCM wakitembea
kwa pamoja wakitoka kwenye mikutano yao ya kufunga kampeni. Ni kielelezo
cha Umoja wetu. Kielelezo cha Utanzania wetu wenye kutofautiana na
wengine.
Ni imani
yangu, ari na moyo huu, tutabaki nao hadi mwisho wa zoezi hili. Maana,
kuna maisha ya kisiasa na kijamii, hata baada ya kukamilishwa kwa zoezi
la uchaguzi.
Nikiwa njiani na makamanda wangu, kwenda kijijini kwetu kupiga kura, nawatakia nyote uchaguzi wa amani.
Maggid
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269