Ndugu zangu,
Afrika
mvua hainyeshi ghafla. Mzee Ali Hassan Mwinyi ni mmoja wa viongozi wa
nchi hii ninaowaheshimu sana. Naamini pia, Rais Mstaafu Mwinyi
anayeheshimika na wengi.
Nilikuwepo
viwanja vya Jangwani siku CCM ilipofanya uzinduzi wa kampeni zake.
Nilimwona na kumsikia kwa masikio yangu Mzee Mwinyi akisema , kuwa kuna
CCM ' A' na CCM ' B'. Na kwama kama CCM ' A' ipo kwanini mchague CCM '
B'.
Kwa
kuangalia kampeni za UKAWA, ndipo maneno ya Mzee Mwinyi yalipodhihiri.
Kampeni za mgombea Urais wa Ukawa zinazohitimishwa leo sambamba na za
CCM, kimsingi zilitawaliwa na Wana- CCM wa zamani.
Ni
viongozi wa zamani wa CCM aina ya Edward Lowassa, Sumaye, Guninita,
Mgeja, Masha, Kingunge na baadhi wengine. Kuna wakati ilikuwa mtu
anahangaika kuitafuta safu ya upinzani ya wapiganaji aina ya John
Mnyika, Godbless Lema, Tundu Lissu, Halima Mdee na wengine. Inatoa
tafsiri pia kuwa, upinzani, hadi miezi mitatu iliyopita, ulikuwa
haujajiandaa kuunda Serikali kwa kutegemea safu yake.
Ndugu zangu,
Duniani
hapa dalili ya mvua ni mawingu. Afrika mvua hainyeshi ghafla. Mwenye
kutamka kuwa mvua imenyesha ghafla, huyo hajajisumbua kuangalia juu
mawinguni. Afrika hata kusanyiko la mawingu ya mvua lina dalili zake.
Wazee wetu wa zamani walikuwa na maarifa ya kuona dalili za kusanyiko la
mawingu ya mvua. Ninachotaka kusema hapa ni hiki; kila jambo ni wakati
na dalili.
Na
tunapokumbushana umuhimu wa kusoma ishara za nyakati hatuna maana ya
kuziangalia saa zetu za mikononi au ukutani. Ni kuyaangalia matendo yetu
ya sasa na hivyo basi umuhimu wa kuzisoma ishara za mambo
yatakayotokea.
Pale viwanja vya Jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM , Mzee Mwinyi alizungumzia juu ya uwepo wa CCM ' A' na CCM ' B'.
Yumkini
moja ya changamoto ya Serikali ijayo ya John Magufuli ni namna ya kuishi
maisha ya kisiasa na kufanya kazi huku kukiwa na upinzani unaotoka kwa
wapinzani asilia, na wale wa kutoka CCM' B'.
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa
Iringa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269