Marekani imeiondoa Burundi kutoka
kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika
kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi.
Katika
barua aliyoiandikia bunge la Congress , rais Barrack Obama ameelezea
kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudia kushuka kwa viwango vya
demokrasia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
''Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano'' Obama.
Obama
alisema kuwa badala ya kuimarika kidemokrasia, Burundi inaendelea
kushuhudia wapiganiaji wa haki za kidemokrasia wakikamatwa na kufungwa
jela huku wengine wengi wakiuawa kwa kudai haki zao za kikatiba
zifwatwe.
Aidha Obama ameelezea kuwa hatua ya serikali ya rais
Nkurunziza ya kuwanyamazisha makundi ya wapinzani kwa kuwashika kuwaua
na hata kuwatesa ni kinyume na maadili ya taifa linalodai kuzingatia
demokrasia.
Marufuku hiyo ya Burundi inaanza kutekelezwa mwezi januari mwakani.
Burundi ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa na kukumbwa na machafuko
punde baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa
tatu kinyume na katiba ya taifa.
Aidha kulitokea jaribio la mapinduzi lakini likazimwa.
Nkurunziza alishiriki uchaguzi huo na akashinda, hata hivyo
kumeendelea kuwa na visa vya maandamano,mauaji na kutoweka kwa
wapinzani wake.
Takriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili
Inakisiwa kuwa watu 200,000 wametoroka makwao na sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.
Mpango
wa AGOA (African Growth and Opportunity Act) ulianzishwa yapata muongo
mmoja uliopita ilikuzisaidia mataifa maskini ya Afrika kuuza bidhaa zao
katika soko la Marekani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269