Mgombea
urais kwa tiketi ya CCM, Dk Pombe Magufuli ametoka jijini
Mwanza kuingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni za lala salama
kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika jumapili hii.
Akiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl julius Nyerere, Magufuli
alikutana na kusalimiana na rais Jakaya Kikwete aliyekuwa
akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Ruvuma kuwaaga wananchi
wa mkoa huo.
Baada ya
hapo Magufuli aliendelea na ratiba yake ya mikutano ya kuomba ridhaa kwa
wakazi wa Dar es Salaam. Maeneo amabyo Magufuli amefanya mkampeni leo
ni pamoja na Kigamboni katika Uwanja wa Machava, Mbagala Zakhiem, Ubungo
Bus Terminal, Ubungo Shekilango, Tandika Mwembeyanga, Uwanja wa TP
Sinza na kumalizia mkutano mkubwa katika viwanja vya Biafra.
Akiwahutubia
wananchi wa Kigamboni, Magufuli aliwatoa hofu kuwa hakuna
atakayedhulumiwa kufuatia ujenzi wa mji wa kisasa katika eneo hilo. pia
alisema eneo hilo atalifanya kuwa wilaya mpya ili liwe na hadhi na
kupewa huduma zote kama jimbo linalojitawala.
Baada ya kuwa wilaya ataipatia Hospitali ya Wilaya na huduma zingine zitaongezwa.
Akiwa
maeneo mengine, Magufuli aliwanadi wabunge na madiwani wanaowania nafasi
hizo kwa tiketi ya CCM huku akiwaahidi wananchi kuwaboreshea maisha,
kupambana na rushwa na mafisadi.
Pia aliongeza kuwa, daraja la Kigamboni linatarajiwa kukamilika mwezi ujao ambapo wananchi watavuka bure.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269