JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 158 KWA MAKOSA YA KUFANYA FUJO, VURUGU NA KUHARIBU MALI WILAYA YA RUNGWE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 38 KWA KUFANYA VURUGU NA UHARIBIFU WA MALI WILAYA YA MBOZI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MNAMO TAREHE 25.10.2015 KUANZIA MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HADI
SAA 16:00 JIONI KULIFANYIKA UCHAGUZI MKUU WA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, WABUNGE NA MADIWANI. KATIKA JIMBO LA RUNGWE, NDUGU
SAUL H. AMON KWA TIKETI YA CCM NA NDUGU JOHN MWAMBIGIJA KWA TIKETI YA
CHADEMA NDIO WALIOKUWA WAKICHUANA VIKALI KUGOMBEA KITI HICHO.
WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIWA LINAENDELEA KUFANYIKA
KATIKA OFISI YA UCHAGUZI JIMBO LA RUNGWE WATU WENGI NA KATIKA HAO
WALIKUWEPO WAFUASI WA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA NDUGU JOHN
MWAMBIGIJA WALIKUSANYIKA NJE YA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE
HUKU NA HAO WAFUASI WA MWAMBIGIJA WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO ZA KASHFA
DHIDI YA MGOMBEA WA CCM, MKURUGENZI WA HALMASHAURI NA JESHI LA POLISI
AMBAO WALIKUWEPO PALE KUHAKIKISHA KUNAKUWEPO HALI YA AMANI NA UTULIVU
WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIENDELEA.
ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI WAFUASI HAO WALIKUWA
WAKIIMBA NYIMBO ZA KASHFA AMBAO ILIONEKANA WAMETOKA WALIOKUWA SEHEMU
MBALIMBALI KAMA VILE RUNGWE, MBEYA MJINI, TUNDUMA NA MAKETE WALIANZA
KUFANYA FUJO NA VURUGU KWA KUWAZOMEA ASKARI NA KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA
MAWE, CHUPA NA FIMBO KWA MADAI YA KUTAKA MATOKEO YATANGAZWE WAKATI
ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIWA LINAENDELEA.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269