Wafungwa 6,000 wameachiwa huru nchini Marekani katika jitihada za kupunguza msongamano katika magereza.
Kwa
mujibu wa idara ya haki ya Marekani mpango huu unawalenga wafungwa
waliopatikana na makosa ya kumiliki , kuuza na ulanguzi wa madawa ya
kulevya.
Hii ndio mara ya kwanza kwa idadi kubwa kama hii ya wafungwa kuachiwa huru nchini humo.
Idara
ya haki inawalenga wafungwa ambao hawana historia ya kutumia nguvu
ambao idadi yao inakisiwa kuwa ni nusu ya wafungwa wote nchini Marekani.
Takriban thuluthi moja ya watu wanaotarajiwa kuachiwa huru ni wageni na hao inatarajiwa kuwa watarejeshwa makwao.
Asilimia kubwa ya wafungwa hao waliachiwa huru ijumaa.
Kundi la pili la wafungwa litaruhusiwa kuondoka jumanne ijayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269