Watu watano, wakiwemo wanajeshi wawili wa jeshi la angani la Uingereza, wamefariki baada ya helikopta kuanguka Afghanistan.
Helikopta
hiyo aina ya Puma Mk2 ilianguka ilipokuwa ikitua katika makao makuu ya
wanajeshi wa Nato mjini Kabul. Muungano huo wa kujihami haujaeleza uraia
wa watu hao wengine waliofariki wala watano waliojeruhiwa.
Msemaji
wa Wizara ya Ulinzi ya Uingereza alisema kuanguka kwa ndege hiyo
kulitokana na “ajali na waa si shambulio kutoka kwa wapiganaji (wa
Taliban)”
Jamaa za wanajeshi wa Uingereza waliofariki zimefahamishwa, wizara hiyo ilisema.
Familia hizo zimeomba muda kidogo kabla ya majina ya wahasiriwa hao kutangazwa.
Ajali hiyo imetokea baada ya msafara wa magari ya kijeshi ya Uingereza kushambuliwa katika mji wa Kabul, Jumapili asubuhi.
Watu saba walijeruhiwa, lakini hakuna aliyefariki.
Wizara
ya ulinzi ya Uingereza imesema bomu la kutegwa lilisababisha ajali
hiyo, lakini maafisa walio Kabul walisema lilikuwa shambulio la kujitoa
mhanga.
Wapiganaji wa Taliban walisema walitekeleza shambulio hilo
kulipiza kisasi mashambulio ya angani yaliyotekelezwa na wanajeshi wa
Marekani walio kwenye muungano wa Nato eneo la Kunduz. Mashambulio hayo
kwenye hospitali ya shirika la madaktari wasio na mipaka MSF liliua raia
na madaktari.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269