Miili ya watu zaidi
mia moja na sitini waliokufa katika ajali ya ndege nchini Misri ipo
njia kuelekea katika mji wa St. Petersburg nchini Urusi.
Katika
ajali hiyo ya ndege iliyotokea siku ya jumamosi huko eneo la Sinai watu
wote mia mbili na ishirini na nne walikuwa katika ndege hiyo walikufa.
Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi ametaka watu wote wawe na uvumilivu wakati uchunguzi ukiwa unaendelea.
Mmoja
wa wachunguzi wa maswala ya anga kutoka Urusi amesema kuwa ndege ya
Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai nchini Misri ililivunjika ikiwa
hewani.
Aleksandr Neradko amesema kwamba mabaki ya ndege hiyo yametapakaa katika rasi ya Sinai.
Abiria
wote mia mbili na ishirini na wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo
,ambao idadi kubwa ni raia wa Urusi,wamefariki dunia,naye mchunguzi
kutoka nchini Urusi amesem akwamba ni mapema mno kutaja chanzo cha ajali
hiyo.
Kikundi cha wanamgambo wa dola ya kiislam mapema wamekiri
kutungua ndege hiyo,madai ambayo yamepingwa na serikali za Urusi na
Misri.nchini Urusi kulikuwa na siku ya maombolezo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269