Wawezeshaji
wa Sheria katika soko la Mchikichini katika Manispaa ya Ilala, wakiwa
na mabango ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi baada ya kuzungumza na
waaandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko
yaliyopo katika Manispaa hiyo kuona maendeleo ya vita ya kupinga
udhalilishaji wa kijinsia katika masoko hayo baada ya Shirika la
Equality for Growth linaloendesha mradi huo kutoa mafunzo kwa
Wawezeshaji wa Sheria wanaoshirikiana na wafanyabiashara katika vita
hivyo.
Mwezeshaji
wa Sheria, Eva Kakobe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili
wa jinsia wanavyokabiliana nayo katika soko hilo.
Mwezeshaji
wa Sheria katika soko hilo, Charles Beatus akichangia kuhusu mwongozo
wa kutoa adhabu kwa wanaobainikwa na makosa ya udhalilishaji. Kushoto ni
Mtaalamu wa kujitolea wa masuala ya kijinsia kutoka nchini Canada,
Ashley Ekelund.
Mwezeshaji wa kisheria katika soko hilo, Domitila Ngwada akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mjumbe
wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko la Mchikichini
Manispaa ya Ilala, Zainabu Namijojo (kushoto), akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao wapo katika
ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe
Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga
udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth
(EfG). Kulia ni Mwezeshai wa Sheria katika soko hilo, Nechi Omar.
Mfanyabiashara wa vitenge na magauni, Sophia Kizinga akichangia jambo kuhusu kupungua kwa ukatili wa jinsia katika soko hilo.
Mfanyabiashara, Ikram Zubery (katikati), akizungumza na waandishi wa habri kuhusu ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Mama Lishe katika soko hilo, Edwiga Assenga (wa pili kulia), akizungumza na wanahabari waliotembelea soko hilo.
Na Dotto Mwaibale
VYUMBA
vilivyokuwa vikitumiwa kwa ajili ya kupimia nguo kabla ya kuzinunua
katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam
vinadaiwa vilikuwa vikitumia kudhalilidha wateja hasa wanawake.
Hayo
yamebainishwa na Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika
soko hilo Zainabu Namijojo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizungumza
na waandishi wa habari ambao wanafanya ziara ya kutembea masoko ya
Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi
ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni
unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).
"Katika
soko letu tulikuwa na changamoto kubwa ya udhalilishaji hasa maeneo ya
wauza nguo kuu kuu (Mitumba), kwani walikuwa wakitumia vyumba vidogo vya
kujaribishia nguo kuwadhalilisha wanawake kwa kuwakamata maungoni na
kuwawekea kioo chini ili waweze kuona utupu wao" alisema Namijojo.
Alisema
hivi sasa vitendo hivyo vimekoma baada ya shirika hilo kufanya
matamasha na semina mbalimbali na kutoa mafunzo kwa baadhi yao ambao
sasa ni Wawezeshaji wa Sheria katika soko hilo ambao wamekuwa karibu na
wafanyabiashara kufuatilia vitendo vya udhalilishaji.
Mwezeshaji
wa Sheria Domitila Ngwada alisema vitendo vya ubakaji na matusi ya
nguono yalishamiri sana lakini hivi sasa hali ni nzuri kwani vitendo
hivyo vimepungua kwa asilimia 70 ukilisha na hapo awali kabla ya
kufikiwa na EfG.
"Tangu
kuwepo na wawezeshaji wa Sheria katika soko letu vijana wengi waliokuwa
na vitendo vya kudhalilisha wanawake wameingiwa na hofu kubwa hasa
kupigwa faini zilizowekwa kuanzia kiwango cha sh.50,000" alisema Ngwada.
Mfanyabiashara
katika soko hilo, Ikram Zuberi alisema jitihada za makusudi zinapaswa
kufanyika ili kumaliza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika sokjo
hilo ingawa kwa kiasi kikubwa vimepungua kwa msaa wa EfG.
Mwezeshaji
wa Sheria katika soko hilo Charles Beatus alisema wale wote wanaopatika
na makosa ya udhalilishaji wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na mwongozo
uliopo na kesi zote zinaanza kusikilizwa sokoni hapo na ikishindikana
upelekwa ngazi nyingine ikiwemo polisi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269