Breaking News

Your Ad Spot

Dec 3, 2015

KAMPUNI YA INTERSWITCH YAZINDUA HUDUMA YA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Interswitch kwa Afrika Mashariki Bernard Matthewman, akizungumza na wadau mbalimbali Dar es Salaam leo , wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo hapa nchini uliofanyika Hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro pamoja na huduma ya malipo kwa njia ya mtandao. 
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Maofisa wa kampuni hiyo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo akiwa katika uzinduzi huo.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.




Na Dotto Mwaibale

Interswitch ni Kampuni Jumuishi inayohusika na masuala ya malipo kwa njia ya mtandao na biashara ikililenga Bara la Afrika na ambayo kwa sasa imeingia kufanya shughuli zake nchini Tanzania kwa ujio na utambulisho wake mpya wa  huduma zake.


Kampuni hii hadi sasa inafanya shughuli zake katika nchi sita zilizopo katika Bara la Afrika na ujio wake katika nchi za Afrika Mashariki kumetokana na kukamilika kwa mpango mkubwa wa utoaji wa malipo kwa mtandao katika Afrika Mashariki ujulikanao kama Paynet Group na kwa sasa Tanzania imeunganishwa na Interswitch.

Shughuli za Paynet hapa nchini ziliaanza tangu mnamo mwaka 2003 ikihusisha utaratibu wa utoaji wa huduma za mitandao ikiwemo ya ATM na M-Pesa ya Tanzania (Vodacom M-Pesa) na Kenya (Safaricom-M-Pesa), na mfumo wa uendeshaji gari kwa kutumia kadi ya EMV kwa nchi za Tanzania, Uganda na Kenya .

Kwa mantiki hiyo, Tanzania inakuwa nchi ya sita katika Bara la Afrika ambayo mfumo wa Interswitch unaanza kufanya  shughuli zake huku ujio na utambulisho wake huo mpya ukilenga thamani na maadili  yaliyopo katika Bara la Afrika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo hapa nchini uliofanyika Hyatt Regency- Kilimanjaro nchini Tanzania Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Interswitch kwa Afrika Mashariki Bernard Matthewman alisema ujio wa kampuni hiyo hapa nchini Tanzania, umelenga kukuza huduma bora za wanazozitoa katika Bara la Afrika.

"Interswitch ni bidhaa mpya  hapa nchini inayotuweka mbali na ushindani wa aina yoyote, lengo letu ni kutoa huduma bora na nzuri kwa wateja wetu ili  kuongeza ufanisi mbele ya wateja wetu kwa kutoa huduma kabambe ndani ya Bara la Afrika kwa kuja na ubunifu wa utakaongeza thamani ya soko.”

“Mikakati yetu ni kufanya upanuzi zaidi katika utoaji wa huduma zetu za malipo kwa njia ya mitandao na biashara kwa ujumla kwa ajili ya soko la Afrika,” alisema Matthewman na kuongeza kuwa;

"Kwa sasa chini ya huduma yetu ya Interswitch tumejipanga imara, tukiwa na miundombinu ya malipo katika maeneo mbalimbali ya Bara la Afrika kwa ajili ya kuharakisha utoaji wa malipo kwa haraka kwa ajili ya kulinda thamani kubwa zaidi kwa washirika wetu na jamii kwa ujumla."

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mawasailiano wa Kanda, Cynthia Kantai alisema ujio mpya wa Kampuni hiyo hapa nchini umelenga kusukuma  kwa kasi utoaji wa huduma mtandao na hivyo kusaidia kukua kwa soko la Afrika tofauti na iliyvyokuwa hapo awali.

Alisema kuwa utoaji wa huduma kwa urahisi, kujali utu, maadili ya uadilifu na uaminifu ndiyo msingi unaosimamiwa na kampuni hiyo.

Tangu ilipozinduliwa wmwaka 2002, shughuli za Interswitch zimezidi kukua kwa kasi na kuchangia katika usafirishaji wa  zaidi ya milioni 350 kwa mwezi na zaidi ya dola $ bilioni 32 kwa mwaka katika shughuli zake.

Aidha kwa mujibu wa Deloitte, Interswitch ni kampuni inayokuwa kwa kasi katika Afrika na ukuaji wa mapato kiasi cha 1226% katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Wakati huo pia , Interswitch pia inatangaza huduma  ya uzinduzi wa kadi ya malipo ijulikanao kama Verve, inayotolewa na Verve International, chini ya kampuni Interswitch Group.

Verve ni kadi kubwa ya malipo nchini Nigeria, ikitoa huduma kwa zaidi ya wateja Milioni 30 ni kadi ya inayohusika na utoaji wa huduma kwa haraka na inayokubalika katika bara la Afrika, hadi sasa inatoa huduma kwa zaidi ya benki 40 barani Afrika.

Uzinduzi wa kadi hii ya Verve kadi katika nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Sudan Kusini na Rwanda utasaidia kutoa katika nchi ya Uganda mahali ambapo tayari inafanya kazi.

Verve tayari pia ipo katika ushirikiano wa kimkakati pamoja na benki za UBA nd KCB kwa kutumia ATM zao wote ATM,  hivyo ujio wake utamsaidia mfanyabiashara kupata huduma zake za malipo katika masoko matano muhimu ya Afrika Mashariki.

Kimataifa kadi ya Verve inakubalika, duniani kote. Mwaka 2013 kampuni mbalimbali zilisaini makubaliano ya ushirikiano na chini ya mpango wa Financial Services (DFS), na kwa sasa kadi hiyo inahudumia kwa zaidi ya mataifa  185 yaliyopo duniani kote.

Kwa upande wake Mkuu wa Huduma wa Kadi ya Verve kwa kanda ya Afrika Mashariki Richard Coate,alisema  kuongezeka kwa utumiaji wa huduma ya kadi hii katika bara la Afrika na duniani kote ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu kwa ajili ya biashara wanayoifanya.
Alisema hatua hiyo pia itasaidia kukuza kukuza uhusiano wa karibu zaidi kibiashara kati ya Afrika Mashariki na Magharibi na kuboresha urahisi wa kufanya biashara katika bara zima la Afrika, na hivyo kuhamasisha ukuaji hata nguvu wa biashara kiujumla.


Interswitch ni Afrika- ni kampuni jumuishi inayohusika na malipo kwa njia ya mtandao na biashara  inayowezesha mzunguko wa fedha kwa njia ya umeme na kuwezesha mabadilishano ya thamani kati ya watu binafsi na mashirika mbalimbali katika msingi thabiti.

Kampuni hiyo ilianza shughuli zake katika miaka ya 2002 ikijihusisha na malipo kwa njia ya mtandao, usindikaji, kampuni ambayo hujenzi wa miundombinu ya malipo na utoaji wa  bidhaa za ubunifu na huduma za kikazi katika bara zima la Afrika.

Interswitch hutoa ushirikiano  katika masuala ya teknolojia, huduma za ushauri, na malipo ya miundombinu kwa serikali, mabenki na mashirika mbalimbali pamoja na huduma kama vile ATM, simu, POS, online (mtandao) na IVR.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages