Ligi Kuu soka Uingereza imeendelea tena usiku wa December 29 kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la King Power, mchezo wa December 29 ulikuwa unazihusisha klabu za Leicester City dhidi ya klabu ya Manchester City.
Uzuri wa mchezo huu ni kuwa vilabu vyote viwili vipo katika mbio za
kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu kutokana na nafasi walizopo katika msimamo
wa Ligi.
Man City walikuwa ugenini kuwakabili wenyeji wao Leicester City, klabu ambayo inafanya vizuri na kuwatishia timu vigogo vya Ligi Kuu Uingereza, klabu ya Leicester City ambayo safu yake ya ushambuliaji ilikuwa inaongozwa na Jamie Vardy na mchezaji wa kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez ilishindwa kutamba katika dimba lake la King Power.
Licha ya kila timu kuonesha jitihada za
kutaka kupata walau goli moja litakaloiwezesha kuvuna point tatu
muihimu, mchezo ulikuwa mgumu na hatimae, dakika 90 zilimalizika kwa
sare ya kutofunga. Pamoja na Man City kuwa na nyota wake kadhaa kama Yaya Toure na Sergio Aguero walishindwa kupenya ngome ya Leicetser City iliyokuwa inaongozwa na Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Robert Huth.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269