Mwenyekiti
wa Soko la Temeke Sterio Amani Mtemi akiwatambulisha wageni waalikwa
katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
yaliyofanyika katika soko hilo Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii
Manispaa ya Temeke, John Bwana.
Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Grace Mathe akisoma risala ya Shirika hilo kwa mgeni rasmi.
Mdau Mwajuma Issa akichangia jambo kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia hasa matusi wanayofanyiwa na wanaume katika soko hilo.
Kijana Andrew Kamtu akielezea chanzo cha ukatili wa kijinsia kuwa kinaanzia kwa wazazi wenyewe.
Ofisa wa EfG, Charles akigawa vitabu vya msaada wa kisherea kuhusu ukatili wa kijinsia.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia kutoka Mkoa wa Kipolisi Temeke wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wakina mama wakiserebuka kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wawezeshaji sheria masokoni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea kutoka kwa kundi la Machozi Theatre Group.
Wananchi wakifutilia maadhimisho hayo.
Ngoma ya mganda ikichezwa ikiongozwa na chipukizi kutoka kundi la Machozi Theatre Group.
Burudani ya Sarakasi hiyo ikifanyika.
Hapa ni furaha tupu.
Mwezeshaji Sheria Kashindye Kapambala akichangia jambo kuhusu ukatili wa jinsia.
Wanawake
wakitembea katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
yaliyofanyika katika Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam leo.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Wasanii
wa Kikundi cha Sanaa cha Machozi Theatre Group wakitoa burudani kwenye
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika
katika Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo
yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa sheria masokoni akichangia jambo kuhusu ukati wa kijinsia masokoni unavyofanyika.
Na Dotto Mwaibale
MASHIRIKA
yasiyo ya kiserikali yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha jamii
kuhusu kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo kusaidia kupunguza
vitendo hivyo nchini.
Hayo
yalibainishwa na Ofisa wa Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Meshack Mpwaga katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili
wa kijinsia yaliyofanyika Soko la Temeke Dar es Salaam leo mchana
yaliyokuwa na kauli mbiu " Funguka chukua hatua mlinde mtoto apate
elimu"
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye maadhimisho hayo yaliyoa andaliwa na
Shirika la Equality for Growth (EfG), Mpwaga alisema mashirika yasiyo ya
kiserikali kwa kiasi kikubwa yameisaidia nchi katika kutoa elimu na
kuhamasisha jamii juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa
kijinsia ambapo uelewa umekuwa mkubwa.
"Uelewa
kwa jamii kuhusu vitendo hivyo ni mkubwa mno wito wangu jamii iendelee
kutoa taarifa polisi pale inapobaini kuwepo kwa vitendo hivyo nasi
tutachukua hatua stahiki" alisema Mpwaga.
Mkuu
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Temeke, John Bwana, ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ametoa mwito kuwa siku 16 za
kupinga ukatili wa jinsia jamii izitumie kuelimishana na kupambana na
ukatili huo wa kijinsia.
Alisema
ni muhimu sasa jamii kuelimika na kuachana na vitendo vya udhalilishaji
sehemu yoyote ili kupata taifa la watu waliostaraabika.
Alisema
serikali hasa idara ya maendeleo ya jamii imekuwa ikisaidia na taasisi
binafsi katika kupiga vita vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia jambo
linalosaidia jamii kufanya shughuli za maendeleo kwa uhuru.
Ofisa
Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Grace Mathe alisema utafiti
uliofanywa na shirika juu ya ukatili dhidi ya wanawake masokoni
unaonesha asilimia 90.32 ya wanawake katika sekta isiyo rasmi
wanafanyiwa ukatili mara kwa mara wa kingono, kimwili na matusi katika
maeneo yao ya kazi.
Alisema
mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya Temeke na Ilala ndani ya masoko
sita ambayo ni Feri, Kisutu, Mchikichini, Gezaulole, Tabata Muslimu na
Temeke Sterio na kuwa umelenga kuwalinda wanawake katika sekta isiyo
rasmi hususani wafanyabiashara masokoni dhidi ya ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269