Meneja
Ustawi wa Jamii na Mahusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa
Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Jumaa Almasi akizungumza kwa niaba ya
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dk, Othman Kiloloma wakati wa
Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo
wazi Duniani 2015, aliomba kuitumia siku hiyo kwa kusheherekea siku hiyo
adhim amabayo nisiku maalum kwa sababu vijana wetu ambao tunawaongelea
leo hi kwetu sisi ni wagonjwa kwa maana yakwamba Tiba yao yote kwa
watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Tiba yao inapatikana
katika Taasisi ya Mifupa Moi, sisi kwa kushirikiana na Chama cha Wazazi
tunakuwa tukifanya kazi bila kuchoka na kwa pamoja kuhakikisha kwamba
hawa watoto wanapata Tiba inayo stail kuhakikisha na wenyewe sikumoja
watapata fulsa yakuwa viongozi na kaulimbiu ya mwaka hu inasema PAMOJA
TUZUIE ULEMAVU WA KUZALIWA, kama tunavyo faham hawa watoto wanavyo
zaliwa wanazaliwa na matatizo na hayo matatizo yanapelekea ulemavu na
unakuwa mkubwa zaidi kama hawatapata tiba stahili kwa hiyo sisi kwa
kushilikiana na Chama tunahakikisha kwamba hawa watotowanaletwa
Hospitali wanapatiwa Tiba bure kwa hiyo na kuwashukuru wafadhili
mbalimbali ambao wanajitolea kufanya kazi kwa pamoja na Taasisi hiyo,
wapo wengi wanao saidia kama AHLAKUL-ISLAMU, akitowa wito Jumaa Almasi,
kuwaomba wazazi kuwaleta watoto ambao bado wanafichwa majumbani ambapo
kwa Taasisi hiyo kwa mwaka hupokelewa watoto 400 hadi 500 kwa mwaka
kwatakwimu walizonazo watoto 4000 kwa mwaka huzaliwa, nakuwasihi wazazi
kuwa wao ni mashuhuda na kuona jinsi Wataalamu watiba wanavyo jitahidi
kuwapatia tiba watoto hao. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA BLOG
Mwenyekiti
na Mjumbe wa Kamati ya kusaidia watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa
na mgongo wazi wakishirikiana na WafanyaBiashara wa Sokoni Kariakoo
Mtaa wa Raha Skweya na Mhonda Jijini Dar es Salaam, Ludovick Mmasi
akizungumza kwa niaba ya wenzake mara walipofika katika Maadhimisho hayo
baada ya kuguswa na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
walipotembelea Taasisi hiyo ya Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo
wazi na kujichangisha na kuwakilisha vitu mbalimbali kama, vyakula vya nafaka, Sabuni, pambas Mafuta na kujitolea Damu na kutowa wito kwa wengine waweze kujitolea kwa hali na mali kuungana kuisaidia
Serikali na isiwe kuiachia kila kitu Serikali hata sisi Wananchi
yatupasa kuguswa tuisaidie Serikali yetu, Mwenyekiti huyo amesema
wanakwenda kujipaka na kusema watapeleka chakua kwa niaba ya Siku Kuu ya X-msa inayo karibia kwaniaba ya wafanyabiashara wenzake
Mtoto Selemani Joseph (14) kushoto ambae ni mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Shule ya Mather Telesia iliyopo Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam akipozi na mwenzake katika ofisi za Chama hicho cha wazizi kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wakati wakijiandaa kuanza maandamano
Wasanii
wa Kikundi cha Sanaa cha Tuamke cha Chanika Dar es Salaam wakitoa
burudani wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa
Kikubwa na Mgongowazi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya Tiba
ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dar es Salaam
Mlezi wa watoto hao na Muuguzi Kiongozi wa Wold ya Watoto hao katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Haulati Daud akiongea jambo wakati wa Maadhimisho hayo
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sikaungu Wilaya ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa Filbert Nyakasi akitowa pongezi kwa waandaaji wa Maadhimisho hayo ambae anamtoto aliyekujanae na kulazwa katika Wodi ya watoto wavichwa vikubwa na mgongo wazi, ambapo mtoto wake anasumbuliwa na uvimbe unaosababisha jicho la kulia kutoka nje, Mtoto wake anaitwa Angelina Malema (12), anaesoma Darasa la Nne Shule ya Msingi Mlanda 'A' Manispaa ya Sumbawanga, Kijiji cha Mlanda Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Manispaa ya Sumbawanga
Mkurugenzi
wa BM Saloon, Benno Chelele, akitoa zawadi katika Maadhimisho ya siku
ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa kikubwa na Mgongowazi yaliyofanyika
katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya
Fahamu (MOI), kwa niaba ya Dorcus Membe ambae alikuwa Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na marafiki zake akiwa ndiye mlezi wa watoto hao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269