Sehemu
ya jengo jipya la TBIII (au terminal III) la uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, likionekana huku ndege moja ya
kimataifa ikipita jirani yake Novemba, 2015. Wadau wa sekta ya usafiri
wa ndege, ambao ni Maafisa Watendaji na Mameneja wawakilishi wa
mashirika hayo walioko hapa nchini, walipata fursa ya kutembelea jengo
hilo Jumatatu Novemba 30, 2015 ili kujionea wenyewe na kupata taarifa ya
maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, litakalokamilika mwakani 2016. Jengo
hilo litakalokuwa na teknolojia ya kisasa katika kuendesha mambo yake
na kuhuduamia abiria, litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6
kwa mwaka mara tatu zaidi ya jengo la sasa yaani Terminal II
linalohudumia abiria milioni 2.5 tu kwa mwaka. Kutokana na ongezeko hilo
kubwa la abiria, wadau hao
wameiomba serikali kupanua Barabara ya Nerere inayoelekea
kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kufuatia kukaribia
kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III au TBIII), la
uwanja huo.
Ombi hilo walilitoa baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya
ujenzi wa jengo hilo.
Akielezea zaidi maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi wa mradi huo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, Mhandisi Mohammed Milanga alisema, jingo la sasa la
JNIA, terminal II, lina uwezo wa kuhuduamia abiria milioni 2.5 tu na kwamba katika jengo jipya, huduma mbalimbali zitapatikana kwa utaratibu utakaowawezesha abiria kufurahia uwepo wao kwenye uwanja huo.
Baada ya kutolewa takwimu hizo, Maafisa hao watendaji
walionyesha wasiwasi wao ni kwa vipi barabara ya sasa ya Nyerere ambayo
huelemewa kwa foleni na itaweza vipi kuwasaidia abiria kufika kwa wakati
kutokana na ongezeko hilo la abiria.
MKUU
wa Idara ya Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA,Bi. Scolastica
Mukajanga, (wapili kushoto), akiwaeleza jambo wadau wa sekta ya usafiri wa
anga, ambao ni Maafisa watendaji wakuu, CEOs wa Mashirika ya ndege wakati
walipotembelea uwanja mpya wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal III
jijini Dar es Salaam, Novemba 30, 2015.Wadau hao wameipongeza TAA kwa mapinduzi
ya miundombinu kwa kupanua uwanja huo mkubwa kabisa hapa nchini na kuelezea
kufurahishwa kwao kutokana na mipango iliyoelezwa na wasimamizi wa ujenzi wa jingo
hilo kuwa utazingatia wadau wote kuwa na ofisi na sehemu mbaklimbali za
kijamii. (Picha na K-VIS Media/Khalfan Said)
Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa jengo
hilo, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akiwaeleza hatua mbalimbali
za ujenzi wa jengo hilo, wadau hao
Msaidizi wa Mkurugenzi wa mradi wa
ujenzi wa jengo la JNIA-TBIII, Mhandisi Caroline Ntambo, (wapili kulia)
kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, akimsikiliza mmoja wa
maafisa wakuu wa shirika la ndege la Qatar Airways, wakati maafisa hao
walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa jengo la TBIII
Maafisa na wahandisi wa TAA
Wakiangalia michoro na taarifa mbalimbali za ujenzi wa jengo
Ziara ya jengo
Picha ya pamoja
Wadau na maafsia wa TAA, wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa jengo hilo iliyokuwa ikitolewa na Mhandisi Mohammed Millanga
Wakati wa maswali na ufafanuzi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269