Na Krantz Mwantepele ,
Ziara
niliyofanya katika Kijiji cha Mwime kata ya Mwendakulima wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mwishoni
wa mwezi Novemba mwaka huu ,ilinipa
mwanga wa jinsi ambavyo wananchi wakiamua kuchukua hatua wanaweza kubadili
mfumo mzima na kuweza kujiletea maendeleo katika Nyanja zote za maendeleo .Kijiji
cha Mwime ambacho wananchi wengi wanajihusisha na biashara, uchimbaji wa madini
na kilimo cha pamba na wapo katika eneo ambalo Barick Buzwagi wanafanya
uchimbaji mkubwa wa dhahabu.
Ofisi za kijiji hicho cha Mwime kilichopo kata ya Mwendakulima wilayani Kahama |
Mgogoro
wa Maslahi wa wananchi wanaozunguka mgodi uliokuwa unamilikiwa na Barrick na
sasa Accaccia uliopo wa Buzwagi kwenye
wilaya ya Kahama katika kijiji cha Mwime kilichopo kata ya Mwendamkulima katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga,
Unaibua mashujaa wa kutetea haki na kudai uwajibikaji u wa viongozi katika
kuendeleza utawala bora na maendeleo kwa ujumla lakini mwishoni inageuka
kuonekana ni maadui wa maendeleo .
Kwa
muda wa miaka zaidi ya mitano sasa
kijiji hiki kimekuwa katika pilikapilika za kuhakikisha wan-aendelea kunufaika
na rasilimali yao ya madini ya dhahabu ambayo kwa sasa yanachimbwa na kampuni
ya Accacia katika mgodi wa Buzwagi
kupitia Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba yaliyosainiwa mwaka 2007.
Kwa
mujibu wa kifungu 1.1 cha Makubaliano ya
Nyongeza ya Mkataba baina ya Kampuni ya Madini ya Pangea kwa niaba ya Barrick
na kijiji; kampuni itakuwa ikikilipa kijiji kiasi cha Tsh milioni 60/- kila
mwaka kwa kipindi cha miaka mitano baada ya uzalishaji kuanza na kisha pande
mbili hizi zitakaa pamoja na kupitia kiwango hiki kwa kadri ya uzalishaji
utakavyokuwa kwa nia ya kuboresha zaidi. Na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi
huu ulianza rasmi mwaka 2009.
Nikiwa
ziarani wilaya ya Kahama nilitembelea
kijiji hiki ambacho mwanzoni mwa mwaka 2007 wananchi wengi wa kijiji cha Mwime
na maeneo ya karibu walijihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu kabla
kampuni ya Pangea kuja kuchukua maeneo hayo kwa kuhodhi mashimo yaliyojulikana
kwa majina ya Zanzibar na majimaji na
kuwafanya wakazi hao kuondoka hapo kupisha uchimbaji wa kisasa,
Mategemeo
ya wananchi kupata maendeleo makubwa baada ya kampuni ya Pangea kuanza
uchimbaji huo wa kisasa yaliendelea kufifia kila uchwao baada ya makubaliano ya
kulipwa kiasi cha milioni 60 kila mwaka
kwa kipindi cha miaka kipindi cha miaka mitano cha uchimbaji
wa madini kutotimizwa kwa wakati.Licha ya kutokuwa na uelekezi rasmi wa
kiseheria wa makubaliano hayo lakini yaliwafanya wananchi wa mMwime kuendelea kuishi maisha
magumu licha ya kuwa mgodi wa Buzwagi kuweza kufanya uchimbaji kwa muda mrefu.
Kuchelewa
kwa malipo kama walivyokubaliana kulisababishwa pia na mapungufu ya uongozi wa
kijiji kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.Sababu nyingine inayotajwa
ni kwa Wanamwime wenyewe kushindwa kudai na kuwahimiza vi-ongozi wao kuchukua
hatua kwa kufuatilia suala hilo.
Bi Maimuna akiwa na mjukuu wake katika duka lake analouza pembejeo za kilimo kwa wakazi wa kijiji cha Mwime |
Mraghabishi
na mpambanaji wa haki za binadamu Bi Maimuna Saidi ambaye pia ni mwananchi wa
kijiji hicho ambaye yeye na wenzake watano walichukua hatua ya kuanza kuhimiza
ufuatiliaji wa pesa hizo kama walivyokubaliana na baada ya mazungumzo marefu na
pia ushirikishaji wa wananchi wote wa kijiji kupitia mikutano ya kijiji
waliweza kufanikisha upatikanaji wa ya
million 300/ kama malipo ya mwaka 2009 – 2013 .
Hivyo Maimuna Said kupitia
ufahamu aliopatiwa alimshawishi Diwani mara kwa mara kuweza kuchukua hatua zaidi,
kwa kuwa yeye alikuwa na mamlaka zaidi.Na mwishowe kupitia harakati mbalimbali
na ushirikishwaji wa wananchi wenzao walifanikiwa kupata kiasi hicho cha pesa.
Pesa
hizo pia zilitumika kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo na huduma za
kijamii kama ujenzi wa miundombinu ya
umeme ,nyumba za manesi, nyumba ya kupumzikia wageni kama kitega uchumi lakini
haya yote yalikuwa kama kipaumbele cha wananchi kufaidikapia kiasi kilichobaki
kulipa baadhi ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao katika upanuzi wa
barabara .
Moja ya nyumba zinazojengwa katika kijiji hiki cha Mwime kama moja ya matumizi ya pesa walizopata kutoka katika mgodi wa Buzwagi |
Huu
mchakato wote usingeweza kufanikiwa kama Wanamwime wenyewe wasingesimama pamoja
na kudai haki yao. Kwa hakika ili tupate tutakachotaka ni lazima tuchukue hatua
za dhati pasipo kuchoka wala kukata tamaa huku tukishirikiana na viongozi wetu
kwani kuna msemo unasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kama dhana
waliotumia wanaMwime wakafanikiwa katika
harakati zao za kujiletea maendeleo
kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269