Mwanamuziki
na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula
kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu onyesho lake
atakalolifanya leo katikka fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es
Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la
Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic
Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa
kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David
Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja
Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele (kushoto), akizungumza
katika mkutano huo ambapo alisema kampuni yao itaendelea kuleta
wanamuziki wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kama walivyofanya
kwa Robarto Amarula.
Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia (kulia), akizungumza na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanamuziki
na mtangazaji wa Redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula
kutoka nchini Zambia, akifanya vitu vyake mbele ya wanahabari.
Mwanamuzi
David Banda 'General Ozzy, akiimba mbele ya wanahabari. Mwanamuziki
huyu atamsindikiza Roberto Amarula wakati wa shoo yao.
Mwanamuziki, Clinton Nyirongo kutoka Zambia naye atakuwepo kutoa burudani. |
Na Dotto Mwaibale
MWANAMUZIKI
wa Zambia anayetamba na wimbo maarufu wa Amarula, Robert Banda ‘Roberto
Amarula’, kesho anatarajia kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika
Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kabla ya
kufanya hivyo mjini Dodoma kesho kutwa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Roberto Amarula, ameahidi kutoa
burudanio ya aina yake kwa wakazi wa Dar es Salaam na Dodoma, akiwataka
mashabiki wa muziki na burudani kujitokeza kwa wingi kwenye shoo zake
hizo.
“Nimefurahia
sana kuja Dar es Salaam na ninaahidi kutoa shoo ya aina yake kesho
(leo) na Dodoma ili kuwaburudisha Watanzania, lakini pia nitatembelea
vituo vya watoto yatima ili kuwafariji na kuwapa nguvu wajione nao ni
sehemu ya jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema
aliyeambatana na wasanii wenzake wa Zambia, David Banda ‘General Ozzy’
na Clinton Ntirongo ‘Mandela’.
Kwa
upande wake, Mkugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba, alisema kuwa shoo
ya leo itawahusisha pia wasanii wa Tanzania kama Ben Pol, Roma
Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengine wengi na kwamba onyesho la
Dodoma litafanyika kwenye ukumbi wa Ngalawa Pub, ikiwa ni sehemu ya
tamasha la Instagram Party.
Kwa
upande wake, Meneja Mawasiliano wa Frecon Ideaz, Krantz Mwantepele,
alisema: “Tunafahamu kiu ya Watanzania katika suala zima la burudani
ndio maana tumewaletea msanii huyu ambaye kwa sasa ni maarufu mno Afrika
na kwingineko tukiahidi kuwaleta wasanii zaidi wakubwa Afrika na hata
Marekani ili kukata kiu ya mashabiki wa muziki hapa nchini.”
Ziara
ya Roberto Amarula ambaye ni mshindi wa tuzo za uandishi bora,
mwanamuziki, mtayarishaji muziki na mtangazaji wa redio, iliyoratibiwa
kwa pamoja na Freconic Ideaz na C&G Solutions, imedhaminiwa na
Millard Ayo, Morena Hotel, Shabiby Bus Servis na Clouds FM.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269